Mambo yakiendelea hivi,mgombea urais ccm lazima atapiga samasoti badala ya push up!

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,142
26,132
Kuna mambo mengi ambayo yalikuwa matarajio kwa awamu ya 5 iwe ccm au upinzani washinde!Mambo hayo makubwa ni:
1.Kufukua na kusafisha kabisa kashfa za ufisadi zilizoitesa nchi ili sasa majeraha yapone na tusonge mbele bila viporo!Kiufupi wananchi walitegemea hakuna jiwe litakalobaki limesimama!

2.Mikopo elimu ya juuande zote mbili ziliwahahakikishia wananchi kuwa wanafunzi wenye ufaulu watapata fursa
3.Ajira
4.Huduma bora za jamii
5.Nk
Mpaka sasa mambo hayo ni kitendawili
Tunakoelekea kuna mtu atalazimika kupiga samasoti kushawishi watu wampe kura!
 
Halafu eti hapa kazi tu!! Kazi gani ajira hakuna, vyeo vime stuck, elimu hoi bin taaban, nk.. Tumsapoti mkulu kwa yale aliyoyafanya yenye manufaa kwetu kama wananchi si manufaa ya kwenye siasa zake, hizo tumwachie mwenyewe
 
Ukiweka sheria pembeni manake unaruhusu utawala wa porini,kila kitu dunia hii kina sheria,hata pumzi tunayopumua(ikiwa polluted kuna kesi)

Binadamu alianza kupata ustaarabu baada ya kujiwekea mazingira ya kuheshimu mambo yanayomzunguka kupitia sheria.

Ukitaka ujue uzuri wa sheria na umuhimu wake,nenda porini uone maisha ya wanyama,kama huwezi kwenda porini,basi angalia sinema za wanyama
 
Mbona unasahau dhuluma kwa watumishi na kunyimwa annual increments na malimbikizo.
Tume huru ya uchaguzi Tanzania muhimu sn idaiwe.
 
Sio samasoti tu, bali analazimika kuwatumia wasaidizi akina Poleporle ili acheze nao sarakasi zile za kujenga minara kama wafanyavyo wachina. Sipati picha mkutano wa kampeni Bukoba mjini hali itakuwaje hiyo 2020.
 
kama huna cha kujifurahisha si utazame hata katuni mkuu. hii post unatujazia server za JF bure tuu wewe.
 
Halafu eti hapa kazi tu!! Kazi gani ajira hakuna, vyeo vime stuck, elimu hoi bin taaban, nk.. Tumsapoti mkulu kwa yale aliyoyafanya yenye manufaa kwetu kama wananchi si manufaa ya kwenye siasa zake, hizo tumwachie mwenyewe

Hapa kazi tu bila akili
 
Halafu eti hapa kazi tu!! Kazi gani ajira hakuna, vyeo vime stuck, elimu hoi bin taaban, nk.. Tumsapoti mkulu kwa yale aliyoyafanya yenye manufaa kwetu kama wananchi si manufaa ya kwenye siasa zake, hizo tumwachie mwenyewe
Wakati mwingine unakuta huyo anaesema hapa kazi tu hana kazi,
Sasa najiuliza huyu mtu ana akili nzuri kweli.

Na Magufuri asivyo na aibu nae anasimama jukwaani na kusema hapa kazi tu!!??
What the https://jamii.app/JFUserGuide..!!!????
Wakati watu hawaajiriwi, watu wamepandishwa madaraja hawajaongezewa mshahara sasa sijui huu ni upumbavu level gani.!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…