Mambo ya kuzingatia unapoenda kumtembelea mteja au unapofanya sales call/visit

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,675
6,046
Katika mambo ya msingi kwenye biashara ni kuhakikisha kwamba unakuwa na wateja.Ili kuweza kuwa na wateja ni lazima uwatafute na unapowatafuta lazima utumie mbinu za uhakika na za kisasa katika kuhakikisha unamfikia mteja wako.

Leo nataka kuzungumzia mambo muhimu ya kuzingatia unapomtembelea mteja wako mahali popote na wakati.Kabla ya kutembelea mteja zingatia iwapo mteja huyo ni mtu ambaye mumewahi kuwasiliana au la,mmewahi kufanya biashara au la,mnafahamiana,hamamiani,unataarifa zake muhimu au la.Hili ni jambo muhimu kwa sababu ndio kigezo chako katika kuweko malengo ya SALES call yako.Unapomtembelea mteja lengo lako klinaweza kuwa ni kufahamiana,kumjulisha kuhusu biadhaa au kampuni,au kumuuzia.Inaweza pia kuwa ni kwa ajili ya kukusanya taarifa nyingine kwa ajili ya kupata market intelligence.

Kulingana na lengo lako kuna mambo muhimu unapaswa kujiandaa nayo ambayo ni pamoja na:
  1. Andaa kabisa mkakati wa mawasiliano na hakikisha unalimit muda utakotumia katika kuhkiksha unafikia lengo lako na mara nyingi isizidi dakika 3.Ndani ya dakika tatu tangu uonane na mteja wako hakikisha umetekeleza lengo lako msingi na umefikisha ujumbe wako.Usimpotezee muda wala usipoteze muda bali hakikisha kwamba ukitumia muda zaidi basi ni katika kuhakikisha unamrdhisha mteja wako na sio ktika kufikia lengo lako.
  2. Andaa business cards za kutosha kulingana na unapoenda na kulingana na idadi ya watu unaowatarajia.na hakikisha business cards zina taarifa zote muhimu kuhusu wewe,nafasi yako n.k.Kama una brochure zozote zile hakikisa unakuwa nazo ambazo ni proffessional
  3. Usijali kuhusu matokeo ila jali kuhusu malengo yako.Kama umetimiza malengo yako basi matokeo yatakuwa sahihi.Ila fahamu kwamba"GOING OUT THERE IS THE BEGINING
  4. Kuwa msikivu sana na hakikisha kila taarifa anayokupatia unaihifadhi ama kwenye notebook au kwenye ubongo wako ili kuhakikisha kwamba unatambua fursa na changamoto kwa mteja husika
  5. Iwapo mteja hatakuwa katika hali ya kuweza kuzungumza na wewe unaweza kufanya miadi wakti huo huo ili kuhakikisha unapata muda mwingine muafaka.Usiwe king'ang'anizi
  6. Mchukulie prospect wako kama vile tayari ni mteja na umhudumie kwa staha na heshima hata kama ataonekana kuwa ni mgumu kuridhisha.Jenga mahusianao mazuri kwani huo ni mtaji wa baadae
Iwpo unahitaji kuwapatia wafanyakazi wako mbinu za mauzo za kipekee basi wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com nasi tutakushauri,kuelekeza na kukupa mbinu za kushika wateja na kuwauzia bidhaa na huduma zako bila shida.Karibu sana tujadili mbinu muhimu za kufanya masoko.
 
Back
Top Bottom