greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,009
Kuna watu wanatamani kuwekeza kwenye soko la hisa lakini hawajui wangalie mambo gani kabla ya kuzingatia kwenye kuchagua kampuni ya kununua hisa zake.
na hili suala lina wakumba mpaka baadhi ya waliowekeza kwenye hili soko,wanakuja kujilaumu baadaye.
Leo tuangalie mambo muhimu ya kuzingatia kwenye Uchaguzi wa kampuni...
1. UTENDAJI WA KAMPUNI HUSIKA KATIKA KATIKA SOKO
Hapa ni utakuwa unaangalia kupanda na kushuka kwa thamani ya hisa za kampuni katika Jedwali ls matokeo linaloandaliwa na Soko la hisa kila siku.
kwenye jedwali hilo unaweza kuona matokeo ya utendaji wa thamani ya hisa kwa siku,kila wiki ,mwezi na hata mwaka mzima.
Hii ndiyo njia maaruf ambayo wengi wenu huitumia.
-pakua app ya D.S.E na utaweza kujionea Jedwari hilo.
2. MWENENDO WA WANAHISA/WAWEKEZAJI WAKUBWA
"Fuata nyuki ule asali",sasa hapa unatakiwa uangalie wapi wawekezaji wakubwa walipowekeza.Hasa anza kwa kuangalia wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi wamewekeza wapi.
Pitia toleo la ripoti ya mwaka ya Kampuni husika na uangalie orodha ya wawekezaji wakubwa/shareholders ,kisha google hayo majina utakayo yaona ujue historia zao na hali zao kiuchumi.
-Kapitie Ripoti ya mwaka ya CRDB,SWISSPORT,TCC na TBL UONE Orodha ya matajiri wazito waliopo kama wawekezaji.
mf.muwekezaji mkubwa wa TBL ni mojawapo ya kampuni kubwa ya bia hapa duniani
muwekezaji wa TCC ni mojawapo ya kampuni kubwa ya tumbaku duniani.
Kwa wawekezaji wa ndani,,nenda uangalie hawa majamaa walipo wekeza.
"Sayeed H. Kadri &/or Basharati Kadri"
3. MIFUKO YA UWEKEZAJI YA PAMOJA NA MIFUKO YA PENSHENI
Hawa jamaa huwekeza kwenye kampuni ambazo wana uhakika zitarudisha faida mfululizo...
nenda tenda kwenye ripoti ya mwaka ya kila kampuni halafu weka alama kila kampuni ambapo utaona mifuko ifuatayo imewekeza
Hapa unaenda kuangalia ukubwa wa thamani ya Kampuni husika...a.k.a market capitalization
ambapo...
thamani ya kampuni= thamni ya hisa moja ya kampuni kwa mwezi husika(mda ) x idadi ya hisa zilizo nunuliwa.
Kampuni unaweza iona ina magari kibao mtaani lakini hapa ikawa chini...
mf
Kwa data za mwaka jana nilizokusanya mpaka sasa...Kampuni ya sigara ya TCC ndiyo kampuni yenye thamani kubwa,ikiwa na thamani ya trillioni 1.7
5. GAWIO
Hili ni rejesho la sehemu ya faida ambayo kampuni imepata kwa mwaka husika kwenda kwa wawewekezaji wake.
Hapa angalio
Kuna makampuni ya uongozi ulio sukika,,Kwa hapa bongo usichanganywe sana na majina ya P.H.D
wewe anagalia kampuni ambalo lina mseto wa uongozi,yaani kuwepo na Wazungu kadhaaa,watu wa Afrika kusini au watu wa Kenya na wachagga kwa mbaaali.
Ila kampuni ni full wabongo mwanzo mwisho,dah pitia taarifa zake mara mbili mbili japo kuna kampuni kama TOL,lipo poa sana
7.MIPANGO YAO YA BAADAYE
Pitia ripoti za kampuni husika ,soma uone kama wanawekeza katika
Katika soko la DSE kuna makampuni ya Upande wa
Uwekezaji wa mda mfupi (1mwaka-3)
hapa utakuwa unalenga sana thamani ya kampuni,labda unataka utumie hisa zako kama dhamana za mkopo.
Uwekezaji wa mda mrefu (7-15 miaka)
Hapa utakuwa unalenga Gawio liwe linaingia kwenye akaunti yako ya benki.
9.KUSOMA RATIO MUHIMU ZA KAMPUNI KATIKA TAARIFA ZA FEDHA ZA MWAKA
Hapa nenda ukasome
EPS=Earning per share
ROE/ROI =Return on Investment/Equity
DEBT TO EQUIT RATIO
PRICE TO BOOK VALUE
PRICE EARNING RATIO
Nime-upload file la Excel ambalo lina taarifa mbalimbali za fedha za makampuni yaliyo orodheshwa DSE kutoka mwaka 2019 hadi 2023...
password : JAMII
NOTICE;
Mimi ni mtaalam wa ujenzi,,ila napenda tusaidiane kupata elimu hii ya masoko ya fedha
kwa wale mlio somea uchumi ,itakuwa Vyema mkawa mstari wa mbele kuchangia,itasaidia sana.
Umaskini ni adui wetu sote.

- UTT
- PSSSF
- NHIF
- ZSSF

- historia ya kampuni kutoa gawio (hufulululiza,au nadra)
- Asilimia ya gawio kwa thamani ya hisa moja,,chukua gawio halafu gawa kwa thamani ya hisa kisha zidisha kwa asilimia
- inajiandaa kujitanua kwa kufungua tawi jipya/kununua mitambo mipya
- Inapunguza madeni iliyokuwa nayo
- Ina jihusisha na kuchangia shughuli za kijamii
- ina hali mbaya kiuchumi
Kuna makampuni ya uongozi ulio sukika,,Kwa hapa bongo usichanganywe sana na majina ya P.H.D
wewe anagalia kampuni ambalo lina mseto wa uongozi,yaani kuwepo na Wazungu kadhaaa,watu wa Afrika kusini au watu wa Kenya na wachagga kwa mbaaali.
Ila kampuni ni full wabongo mwanzo mwisho,dah pitia taarifa zake mara mbili mbili japo kuna kampuni kama TOL,lipo poa sana
7.MIPANGO YAO YA BAADAYE
Pitia ripoti za kampuni husika ,soma uone kama wanawekeza katika
- utafiti
- Ununuzi wa mitambo mipya
- kuongeza matawi
- uboreshaji wa mazingira rafiki ya kazi kwa wafanyakazi
Katika soko la DSE kuna makampuni ya Upande wa
- Fedha na benki e.g NMB,CRDB,MKOMBOZI na NICOL
- Ujenzi e.g TWIGA
- Viwanda e.g T.O.L
- Usafirishaji e.g SWISPORT na PRECISION
- Mawasiliano e.g VODACOM
- Mafuta e.g SWALA
- Bidhaa za starehe e.g TBL na TCC
- ,watanzania wanapenda starehe hasa kunywa,,jibu ni ndiyo tena sana
- ni watu wa kutumia usafiri wa ndege,,jibu hapana
- ni wakopaji,,,tena sana,na wakikopa wanaenda kwenye starehe na ujenzi