Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,269
- 14,693
Nipo safarini,tena safar ndefu imeanza saa kumi nafika kesho asubuhi inshallah,sasa kwa safari kama hii unatarajia seat mate wako atakuwa mwanamke,nimechill dirishani kabisa natarajia jirani atakuja dem eeh anakuja mwamba mpaka nimechoka
Sijui tutaongea nini na huyu mwamba,hapa sana sana story za chadema na mengine ambayo ambayo yatafanya safar izidi kuwa ndefu,lkn ukiwa na mchuchu pembeni walau safar inakuwa na mvuto,sio lazima muwe kimapenzi zaidi laa,ila kuna raha fulani ukiwa safar ndefu na dem pembeni yako mnaweza fanya hata meditation ya hisia
Si unajua usiku mara umelaliwa kwenye bega mara unasikiliza mastory basi safar inakuwa fupi kiasi fulani
Yani mwaka naona umeanza kimachale sana kwa upande wangu,halafu kibaya zaidi ukicheki siti nyingine napo wamekaa warembo watupu,natamani tubadishane mimi niende kule na mmoja aje kwa huyu mwamba
Anyway nikifanikiwa kubadilisha siti nitawaambia,mkiona kimya ujue mambo ya network si unajua road network inahama hama
Ni hayo tu!