Mambo Makuu yanayoonyesha aliyembele yako ni mwanamke wa shoka pamoja na Sifa za Mwanamke bora anayejitambua

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
28,962
69,588
MAMBO MAKUU YANAYOONYESHA ALIYEMBELE YAKO NI MWANAMKE WA SHOKA. SUPER WOMAN; SIFA ZA MWANAMKE BORA ANAYEJITAMBUA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Ni kweli mwanamke Bora,mwema na super woman hutoka kwa MUNGU. Yaani huwezi mpata kwa Njia yoyote bile kupewa na MUNGU. Na hii ndio inafanya Wanawake wa shoka kuwa nadra Sana na Wachache Sana.

Wanawake wote wa Tibeli wenye kupenda HAKI, KWELI, maarifa na ufahamu, na wenye upendo ni wanawake wa shoka.

Zifuatazo ni sifa za Wanawake wa shoka, wanawake wanaojitambua, wanawake Bora;

1. SIO TEGEMEZI ILA NI WASAIDIZI WA WAUME ZAO.

Mwanamke wa shoka kamwe hawezi kuwa tegemezi kwa mwanaume kama mtoto mdogo Bali huwa Msaidizi wa mumewe. Msaidizi Kihisia, Kimwili, Kiroho na kiakili. Huyo ni mwanamke.
Sio mwanamke azae tuu ndio afikiri amemaliza.

Jamii nyingi ambazo ni Maskini tatizo kubwa huanzia kwa Wanawake kuwa tegemezi. Au kuna mfumo ambao unamfanya mwanamke kuwa tegemezi.

Mwanamke wa shoka hawezi kukubali majukumu yake yaishie kwenye kuwa kiwanda cha kuzalisha watoto kama incubator.

2. Afanye Kazi ya uzalishaji na aweze kujitegemea na kuendesha maisha yake.
Mwanamke ili awe mtu na heshima yake ilindwe na UTU wake uheshimiwe lazima afanye Kazi na ajitegemee.
Aweze kuendesha maisha yake pasipo kumtegemea mwanaume. Aweze kulea watoto wake hata mumewe akifa. Huyo ni mwanamke wa shoka. Mwanamke Bora na ndio Binti za Tibeli walivyo.

3. Hakubali Kuonewa na hakubali kumuonea Mtu. (Mtenda HAKI)
Sio kwa Sababu mtu ni Mumeo ndio akuonee. Hata hivyo ni ngumu kumuonea mwanamke anayejitegemea.

Mwanamke wa shoka hujiheshimu na kuheshimu wengine. Hadhulumu Haki za watu na Wala yeye hakubali kudhulumiwa. Huyo ni mtibeli.

Unamheshimu atakuheshimu. Unamdharau atakudharau. Huyo ni mtibeli.

Haki ndio inayomuongoza. Ukimuoa ukiwa kama Mume lazima ukubali kutenda HAKI. Vinginevyo picha itaungua mapema na hatakuwa na hasara kwa Sababu anauwezo WA kuyaendesha maisha yake bila ya wewe. Kazi anafanya, anauwezo WA kujilisha na kulisha watoto wake bila utegemezi wa yeyote. Hiyo ni Binti wa Tibeli
Na mambo haya hafundishwi bali yapo automatic.

4. Baraka alizojaliwa hazimfanyi adharau na kuwadhulumu wengine.
Yeye huongozwa na kanuni Ile isemayo, mpe mtu kile anachostahili, HAKI.
Mwenye kuheshimiwa atamheshimu. Mwenye kudharauliwa (asiyemuadilifu) atamdharau.

Binti za Tibeli hata awe na pesa Kiasi gani hawezi kumdharau mumewe Kisa Pesa zake. Bali ataanza kumletea mumewe dharau akianza mambo ya kipuuzi na uonevu. Mfano, mwanaume kufanya Umalaya uliopitiliza Binti za Tibeli hawatakuvumilia na lazima wakuonyeshe dharau na kukunyoosha kidogo. Usipobadilika lazima waombe Talaka.
Ni kweli mwanaume anatamaa lakini kuwa na tamaa kuliko pitiliza na Umalaya wa kijinga hautavumiliwa.

5. Lazima awe Msafi
Mwanamke wa shoka huwezi kumkuta analala hovyohovyo na wanaume kama mbwa.
Uchi wake sio shimo la manii za wanaume. Mwanamke Bora ni Msafi na anakinyaa. Hawezi Kulala na mwanaume zaidi ya Mmoja.

Akishakuwa na mahusiano na X atakuwa na huyohuyo Mpaka waachane iwe kwa Kifo au Talaka. Na sio yupo na X lakini Kesho kutwa akija Y na Z wanamwaga takataka Zao.

Usafi wa Mwili,
Huwezi mkuta anauharibu mwili kwa kuchora mavitu ya hovyohovyo yasiyoeleweka.
Au kuvaa mavazi yanayotweza UTU wake.
Kukaa uchi maeneo yasiyo sahihi ni uchafu.
Hawezi kuongea matusi au Maneno machafu kupitia mdomo wake. Huyo ni mwanamke Bora.
Mavazi anayovaa yanaendana na umri wake, hadhi yake, na mazingira.

6. Hawezi kuwa mshirikina au mchawi

Kuamini katika ushirikina ni udhaifu WA Hali ya juu kabisa kwa mtu yeyote Yule sio tuu mwanamke Bali hata mwanaume.

Mwanamke wa shoka huwezi kuta anaenda kwa waganga wa kienyeji wenye Imani potofu au kuwa mchawi.
Ukiona mwanamke yeyote mshirikina au mchawi ujue hapo hamna kitu bila kujali nafasi yake. Huyo ni mwanamke dhaifu tuu.

7. Haingii kwenye mahusiano kwa Sababu ya Kutaka huduma ya Mwanaume au pesa.
Binti za Tibeli au wanawake wa shoka huingia kwenye mahusiano kwa Sababu ya Upendo wa dhati. Mapenzi ya kweli.
Ni kwa sababu wao wenyewe wanajiweza na wanaweza kuendesha maisha yao kwani wanafanya Kazi za kuingiza kipato.
Wanaridhika na kipato

Huwezi mnyanyasa Binti wa Tibeli kwa Sababu yeye ni mtu. Hahitaji Msaada wa serikali au Haki za Binadamu kwa Sababu anajiweza. Yeye sio mlemavu au mhanga.

Mwanamke asiyeweza kujitegemea kamwe hawezi kuwa na upendo wa dhati.
Ili mwanaume apate mapenzi ya KWELI ni lazima atafute mwanamke WA shoka ambaye atampenda kwa upendo wa dhati.

8. Mwanamke wa shoka hatakubali kuwa Mzigo kwa mumewe.
Yaani alishwe kama Mgonjwa yeye kakaa tuu kama anastroke.
Binti za Tibeli Wana Aibu. Na mojawapo ya aibu ya mwanamke mwenye UTU ni kuwa Mzigo kwa mtu mwingine.

Kwa mwanaume anayejielewa huogopa Sana kuoa au Kuishi na Mwanamke asiye na Aibu.
Yaani mwanamke anaona kawaida kulishwa, kuvalishwa, kupewa kila kitu yeye anatoa macho tuu. Ni kwamba mwanamke WA Aina hiyo Hana akili, Hana aibu, na ni Hatari kwa future ya Mwanaume.

Binti za Tibeli Wana Aibu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom