(1) Kalenda ya Korea Kaskazini inategemea mwaka wa kuzaliwa wa mwanzilishi wa nchi hiyo, Kim Il-Sung. Mwaka huu 2023, Korea Kaskazini itaadhimisha mwaka wa 112, kwa vile Kim Il-Sung alizaliwa mwaka 1912.
(2) Korea Kaskazini ina mfumo wake (operating system) kwenye upande wa computers zao, unaoitwa Red Star OS. Ni toleo lililorekebishwa la Linux na limeundwa ili kuwaweka watumiaji wote ndani ya nchi chini ya uangalizi.
(3) Korea Kaskazini ina time zone yake, inayojulikana kama ''Pyongyang Time'', ambayo iko dakika 30 nyuma ya Korea Kusini na Japan.
(4) Serikali nchini Korea Kaskazini imepiga marufuku mitindo fulani ya nywele, zikiwemo nywele ndefu za wanaume na mitindo fulani ya wanawake. Inasemekana kuna mitindo 28 pekee ya nywele iliyoidhinishwa na serikali kwa wanawake na 10 kwa wanaume.
(5) Nchini Korea Kaskazini, ni lazima kuvaa beji yenye picha ya mwanzilishi wa nchi hiyo, Kim Il-Sung, na mwanawe, Kim Jong-Il. Kukosa kufanya hivyo kunaweza kusababisha adhabu.
(6) Korea Kaskazini ina jeshi la watu milioni 1.2, ambayo ni ya nne kwa ukubwa duniani. Hata hivyo, nchi hiyo pia inajulikana kwa kuwa na vifaa vya kijeshi vilivyopitwa na wakati na visivyotunzwa vizuri.
(7) Korea Kaskazini ndio nchi pekee duniani kuwa na udikteta wa kikomunisti wa kurithi. Nchi hiyo imetawaliwa na familia ya Kim kwa vizazi vitatu, huku kiongozi wa sasa akiwa Kim Jong-Un.
(8) Korea Kaskazini ni moja ya nchi maskini zaidi duniani, wastani wa Pato la Taifa kwa kila mtu ni karibu $1,800 pekee. Licha ya hayo, serikali inaripotiwa kutumia sehemu kubwa ya bajeti yake katika mpango wake wa kijeshi na silaha za nyuklia.