Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 1,660
- 4,586
Mambo 5 ambayo MWANAMKE hutakiwi kuficha pale unapoanza MAHUSIANO!
(1) Umri wako; Kuna wanaume wanajali kuhusu umri, najua unaogopa labda ukimuambia ukweli atakukimbia, ila jua kuwa ipo siku ataujua ukweli, kwa maana hiyo muambie mapema, ili asije kukuacha tayari ushampenda na ushapoteza muda wako.
Si lazima umuambie siku ya kwanza kama hajakuuliza kwani wengine wanaweza kushtuka na kukuacha, muache akujue kwanza, labda hata mwezi kisha tafuta namna ya kuingiza umri wako hasa kama unahisi wewe umemzidi umri!
(2) Una Mtoto/Ulishawahi kuzaa; Hii ni mapema kabisa mwezi wa kwanza wa Mahusiano, kuna wanaume walishajiwekea hawaoi wanawake wenye watoto, ni maamuzi yao. Ukichelewa kumuambia labda mshaingia kwenye ndoa, kuna mawili, anaweza kukuacha hapohapo au akabaki na wewe ila asimpende mwanao, ukibahatisha la tatu atakusamehe na kukubali kuishi nawewe ila si vyema kudanganya!
(3) Ulishawahi kuolewa au bado uko kwenye ndoa ila mmetengana. Si lazima kumuambia siku ya kwanza, ila usiubiri hata mwezi kwa maana utaanza kumpenda, ukweli nikuwa, hivi vituvinajulikana kirahisi, atakuja kusikia kwa rafiki zako, ndugu na watu wengine, sasa ukidanganya kuna uwezekano akaja kukugeuka.
(4) Dini yako; Hata kama uko tayari kubadilisha kumfuata lakini anapaswa kujua kuwa wewe ni dini gani? Pia umuambie na misimamo yako kuhusu kubadilisha dini kama mko dini tofauti, zungumzia hii ishu mapema kwani ni kubwa, mwanzo unaweza usione kama ni shida ila baadaye ikakugharimu.
(5) Kabila; ajue kabisa ili asije kusema “Kwetu hatuoei wapare!” Wakati mwingine kama mmetofautiana kuhusu makabila muulize kabisa ili ujue kama kwao ishu ya yeye kuwa na mahusiano na kabila jingine sio shida. Usimuulizie ndoa bali mahusiano, ili baadaye akija akitaka kukuacha akuache kwakua mmechokana sio mnakaa miaka 7 ndiyo anakuja kusema kwetu hatuoi ‘Watu wa Kasikazini!”
#sweetpain