Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 15,802
- 33,529
(1) Kusikiliza matatizo ya Marafiki zao na kuyabeba na wasiwasi. Una rafiki yako anafanyiwa vitu vya ajabu na mwanaume wake, kila siku anakuambia na wewe unaanza kujihisi kama unasalitiwa, huwaamaini wanaume na moja kwa moja unaanza kumpima mpenzi wako kwa kuangalia rafiki yake, unakua na hasira, kisirani na vitu kidogo unakasirika, anakuchoka kwani hajui kakukosea nini kumbe zilikua ni mambo za rafiki zako!
(2) Haraka ya maisha, ushaambiwa huko mtaani kuwa ukifikisha miaka 28 unatakiwa kuzaa, ushadanganywa kuwa miaka 30 na ngapi huko itakua ngumu kupata mtoto, basi moja kwa moja unaanza kelele kwa mpenzi wako. kwanza unataka ndoa lakini pili unataka afanikiwe kama mume wa dada yako. Mwanaume hana kazi au ndiyo kapata kazi hata mshahara hajalewea, bado anasaidia ndugu zake, bado hajajipanga unaanza habari za viwanja.
Unamlinganisha na kila mtu, unamuona mzembe hayuko siriasi na maisha, kila siku unalalamika hakuhudumii, unataka vitu ambavyo rafiki zako wanapewa na wababa wa miaka 50, unamsumbua mpaka anakuacha wakati alikua na malengo mengi.
(3) Kutokukubali kukua; Mwanzoni mwa mahusiano mwanaume alikua anajali sana, kupiga simu mara kumi, meseji mara kibao, kila dakika kutoka pamoja na mambo kama hayo. Sasa mambo yanabadilika, kwanza mnazoeana na pili umri unaenda, kuna mambo yalikua ya maana mkiwa na miaka 25 lakini sasa mna miaka 30 mambo hayo yanaonekana kama ya kitoto kwa baadhi ya watu.
Sasa mwanaume kabadilika, hatumi meseji kama zamani, kupiga simu kama zamani anakua bize na kazi kawa mtu mzima mwanamke yeye hataki kukua, anataka mwanaume ambaye wana miaka 3 wachart kama ndiyo anamtongoza.
Hapo anakutana na kakijana, ofisini, dukani au bodaboda, anampa namba ya simu, anaanza kumchatisha, kumsifia, kumuona kama malaika, anamsahau mchizi aki mini huyu ni tofauti bila kujua ni kama nguo mpya kabla ya kuifua inakukaa lakini ukishaifua inaanza kukupwaya.
Mwanaume mpya anajali mara mia ila naye akishakuzoea anaacha anakua kama wa zamani si kwakua hakupendi bali kwakua kakua, umri umeenda na ashakuzoea. Wanawake wengi husaliti watu wao wakidhani wamebadilika kumbe nyakati ndiyo zimebadilika!