Mama Mkwe anataka majina yangu matatu

Mabula Msirikale

JF-Expert Member
Nov 29, 2022
638
1,499
Habari ya weekend JF.
Mpenzi wangu nimempa ujauzito.
Nipo mbioni kupeleka posa kwao ili nifunge nae ndoa Takatifu.

Wazazi wake bado sijakutana nao, binti yao ameshampa taarifa mama yake kuhusu hali yake ya ujauzito, mama yake akamuuliza kama kama anatunzwa akajibu ndiyo.
Sasa leo asubuhi mpenzi kanipa taarifa ya kushtua anasema mama yake kampigia simu anataka yeye (binti) amtumie majina yangu matatu, ya baba yangu matatu pia majina na mama yangu matatu.

Mama kijacho wangu kasema hawezi kumtumia kakataa japo hajamtamkia mama yake kua hatomtumia hayo majina.

Wadau huyu mama mkwe wangu mtarajiwa anataka hayo majina ya nini? Humu kuna wajuzi wengi naomba kujua anachotaka.
 
Wewe chukulia kawaida haya maisha ukianza kufuatikia Kila kitu utapata shida tu kama mama kijacho mpo naye poa mengine ni ya ziada.
Mimi siogopi maana namtumainia Mungu. Mwanzo nilikua na plan za kumtumia mama mkwe nauli binti yake atakapokaribia kujifungua aje . Kwa hili la leo mmh nimegairi mtoto wangu si atakua anaoga madawa tu.
 
Back
Top Bottom