BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,111
Kamati kuu ya CCM imewavua nyadhifa zao viongozi wakuu wa umoja wa vijana baada ya viongozi hao kukubali uteuzi wa nafasi nyingine. Viongozi hao ni Mwenyekiti Kheri James, Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid na Katibu mkuu Raymond Mangwala.
Kamati kuu imewavua vyeo vyao kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CCM no.22 toleo la mwaka 2020 ambazo zinazuia kiongozi kuwa na nafasi mbili (kwenye chama na serikali). Tayari nafasi ya Katibu Mkuu imejazwa na Kenani Kihongosi, na nafasi nyingine zitajazwa baadae.
#MyTake:
Mama anaendelea kuupiga mwingi. Anapanga safu yake kwa akili kubwa sana. Akina Kheri James walipoteuliwa kuwa MaDC hawakujua ni mtego. Wakakubali "kichwakichwa" na hatimaye wameliwa vichwa.
Mkiti wa UVCCM hata Katibu wake ni fursa kubwa kuliko UDC. Mkiti anaingia kwenye vikao vya Kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. Katibu anaingia kwenye vikao vya sekretarieti. Hakuna siri yoyote ambayo Rais ataongea kwenye chama bila kujua. Akiongea kwenye Kamati kuu Kheri atasikia na akiongea kwenye Sekretarieti Raymond atasikia.
Sasa mama amewapiga kanzu. Kuanzia leo Kheri hatakaa ajue chochote kinachojadiliwa na CCM taifa. Atasikia mambo ya CCM Kibangu au Kibamba kwa mangi ambapo ndio wilaya aliyopewa kuongoza. Na huko pia hana uhakika kwa sababu muda wowote mama anaweza kumtengua akitaka.
Kwahiyo mdogo wangu Kheri yupo kwenye wakati mgumu sana. Angekua na uwezo angeomba siku zirudi nyuma aukatae UDC ili abaki Mwenyekiti wa vijana, nafasi ambayo ilimpa fursa nyingi ambazo hawezi kuziota akiwa DC.
Mabilioni ya bajeti ya UVCCM yalipita kwake kwa ajili ya approval. Miradi yote inayosimamiwa na UVCCM kuanzia lile ghorofa la vijana pale Lumumba hadi zile fremu za kitimoto pale Iringa, ilikua chini yake.
Kheri alikua anaogopwa na Wabunge viti maalumu wa UVCCM kuliko wanavyoogopa Corona. Hii ni kwa sababu yeye ndiye alikua anapitia mkeka wa wagombea na kukata majina. Leo hawezi kukata jina hata la mgombea udiwani.
Mwaka jana nilikutana na msafara wa Kheri mkoani Shinyanga. Polisi barabarani wamejipanga kwa nidhamu eti M/kiti UVCCM anapita. Alipewa ulinzi mkali na king'ora kilimuongoza. Leo vyote vimeyeyuka kwa kutegwa na UDC. Mama anaupiga kama Ng'holo Kante.!