Mama afariki wakati madaktari wakikataa kuokoa mtoto

Balungi

JF-Expert Member
May 25, 2011
234
162
Nimesikitishwa sana na kufariki kwa mama mmoja wiki mbili zilizopita, ambaye alikuwa mjamzito katika kijiji cha Nam-bali, Newala mkoani Mtwara baada ya kupata homa iliyopelekea kupelekwa zahanati ya kijijini hapo. Baada ya hali kuendelea kuwa mbaya, alikimbizwa kituo cha afya Chihangu kwa matibabu zaidi lakini alifariki na mtoto aliendelea kucheza tumboni. Ndugu wa mama, waliwaomba marehemu apasuliwe ili kuokoa mtoto aliyekuwa anacheza ila madaktari walikataa kabisa hali iliyopelekea mtoto naye kukosa hewa na kufariki
 
Walikataa kwa kutoa sababu gani? Hilo ndio jambo la msingi kujua!
 
Muda mwingine inahitaj kufanya maamuz magum kwa kutumia akil ya kuzaliwa...ila naona hao walipigwa ganzi tu.
 
Walisema kuwa hawaruhusiwi kufanya hivyo
Mkuu kama ni hizi dispensary ndogo (vituo vya afya) amabvyo hawaruhusiwi kufanya upasuaji inawezekena wakawa na hoja ya msingi. Unajua utabibu una miiko yake na imewekwa kwa sababu maalum.
 
Mkuu kama ni hizi dispensary ndogo (vituo vya afya) amabvyo hawaruhusiwi kufanya upasuaji inawezekena wakawa na hoja ya msingi. Unajua utabibu una miiko yake na imewekwa kwa sababu maalum.
Kama ni hivyo basi ni mtihani kwa walioko vijijini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…