Mali ya dhuluma haimfikii mkujuu, hayo ni maneno ya wazee

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Neno analolisema mzee aliyekuzidi umri siku zote ni la kusikilizwa kwa umakini. Nimewahi kumsikia mzee mmoja akisema kuwa mali ya dhuluma huwa haimfikii mjukuu. Alimaanisha kuwa kisicho haki kinapochumwa na mtu ni sawa na yule mtu kuwashikia wenye mali, anaweza kukaa na hiyo riziki isiyokuwa yake kwa miaka mingi lakini ipo siku mali hiyo itawarudia wale wenye haki ya kuimiliki.

Huwa nawaangalia matajiri ambao wanaibuka kadri ambavyo awamu za uongozi zinavyokuja na kuondoka. Waliibuka matajiri wa awamu ya kwanza, ilipoondoka na kuja ile ya pili wale walioshi kwa dhuluma katika awamu ya kwanza wakafilisika. Ikaibuka awamu ya pili, na wale walioshi kwa kuwadhulumu na kuwaona walio wengi katika awamu ya kwanza, ikawa ni zamu yao kufilisika. Ikaja awamu ya tatu na matajiri wake, wale waliotesa katika awamu ya pili wakaanza kuingia katika maisha ya dhiki tofauti na ile miaka kumi ya starehe waliyoizoea. Awamu ya nne ikaja, wakaibuka matajiri "wazee wa vimemo", wakati wale matajiri wa awamu ya tatu wakizidi kufilisika. Sasa tunayo awamu ya tano, ambayo na yenyewe itakuwa na matajiri wake wa miaka kumi.

Lakini wapo wale matajiri ambao wanaishi kwa amani katika awamu zote bila ya kuhofia mamlaka za kiserikali kuja kutaifisha mali zao. Utajiri wao unawafikia wajukuu zao, ambao wanakua wakifurahia mali iliyopatikana kwa amani. Mali ya dhuluma hufurahiwa na watoto, huwa haiwezi kumfikia mjukuu kwa sababu aliyedhulumu ni kama vile amevaa nguo ya kuazima, kuna siku mwenye mali atakuja kuifuata.

Na haya ndio maisha ya kiafrika. Wapambe wa serikali zinazokuwa madarakani wanafurahia maisha wakifahamu fika kuwa uongozi unaofuatia sio mzuri kwao. Wapo matajiri wachache wenye kutokea jasho walichonacho, hawa mali zao zinarithiwa mpaka na vitukuu lakini wapo wengi ambao utajiri wao hauwafikii wajukuu zao kwa sababu walichonacho ni dhuluma, kimepatikana huku wanyonge wakitoa machozi, wanyonge wakiwa na vinyongo mioyoni. Maneno ya watu wazima kwa maana ya Baba zetu na Mama zetu yamejaa busara sana. Mali ya dhuluma haimfikii mjukuu.
 
chavda
bakhresa
jitu patel
dewji
.
.
.
.
mengi

kuwanakili kwa uchache, si haba kuhusishwa na tuhuma japo haziwafilisi. utajiri wao utavuka vizazi vinne!

wafanyabiashara wana fedha, watawala wanahitaji fedha, ni madalali wa kukusanya Kodi kwa niaba ya serikali hivyo mahusiano yao yanamuumiza mwananchi ni nadra kuumizana serikali na wafanyabiashara hizo ni mbwembwe za muda.
 
Maneno kuntu ya mtoa mada,wadokozi hawatachangia. Kwa tunaoiamini Biblia kama kitabu kitakatifu cha MUNGU ina mistari mingi kuhusu mali inayokuja haraka .Ni Baraka kuwa na mali bora mali hiyo isiwe maudhi kwa MUNGU na wanadamu jinsi ulivyoipata na unavyoitumia. Ahsante kwa ujumbe mzuri.
 
Hao wote wapo na walikuwepo ktk serikali ya ccm
 
Wacha chuki zako kwa mengi
 




Mkuu hapa pia unataka kututhibitishia ya kwamba hata ile chenji yetu ya rada wakati wa Mkapa hawatatumia wajukuu zake? Bila ya kusahau na chenji yetu ya ESCROW kwa akina Chenge, Muhongo, werema naTibaijuka vipi?. Jee Maaskofu nao walipewa kwenye mgao wa ESCROW nao wamo pia humo ama dhambi hii inawahusu matajiri pekee! Tunaomba ufafanuzi mkuu maana wengine tu wajukuu wa maaskofu na tunaogopa kula dhambi!
 
Chenye baraka kwa mtu ni kile kinachomtoa jasho, ni kile ambacho hata akikipata anakwenda kulala usiku akiwa na amani moyoni mwake. Kama hizi pesa unazozitaja haziwapi amani hao wahusika wa kashfa ulizozitaja maana yake hiyo ni mali ya dhuluma.
 
Fedha ya dhuluma ipo CHADEMA pia, kuna ile hela ambayo mzee Slaa aliihangaikia ije kutoka kwa wafadhili, halafu wenye chama chao wakaipindisha njia ikarudi kule kule nje ilipotoka, na hiyo nayo haimfikii mjukuu. Dhuluma ipo kila upande, CCM na CHADEMA. Kuna ile fedha ya richmond, ambayo ilimfukuzisha mtu kazi kiasi ambacho akasimama bungeni na kutangaza kujiuzulu, ile pia haiwezi kumfikia mjukuu kwani ni pesa chafu, watu waliishi bila ya umeme kwa miezi mingi tu, kumbe kuna wapigaji walikuwa kazini na kuwasababishia umasikini walio wengi.
 


Mkuu naona umeamua kumeonesha sura yako halisi! Kwamba unatetea dhuluma! Sasa vipi hii dhuluma ni lazima iwe ni fedha tu ama siasa na uongozi pia kuna dhuluma? Mkuu naomba unieleweshe kondoo wako.
 
Mkuu naona umeamu kumeonesha sura yako halisi! Kwamba unatetea dhuluma! Sasa vipi hii dhuluma ni lazima iwe ni fedha tu ama siasa na uongozi pia kuna dhuluma? Mkuu naomba unieleweshe kondoo wako.
Ha ha ha, nimegusa penyewe kaka, siasa na uongozi kwa pamoja vikitumika vibaya ni mwanzo wa mtu kujijazia mikosi kwenye maisha yake. Mobutu alikuwa anaua watu kama vile mtu anavyovaa shati au suruali, lakini alipokufa alizikwa na watu wasiozidi 20. Alikuwa ni bilionea lakini mali zake kwa sasa hazijulikani zinamfaidisha nani. Sitetei dhuluma najaribu kujenga hoja.
 
Mkuu umeongea maneno ya busara sana . Kwahiyo tunaweza kusema pia serikali za awamu zote zilizo dhulumu rasilimali za watanzani kwa kuwapa wageni nakufanya nchi shamba la bibi. Kodi na mapato waliyo kusanya kidogo hakuweza kumfikia mjukuu wa awamu ya tano . Kweli nimekubali mali ya dhuluma mjukuu hato ambulia kitu ndio sisi wenyewe tunao lia Leo maisha magumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…