RIGHT MARKER
Member
- Apr 30, 2018
- 88
- 336
💼MHADHARA WA TISA (9)
Siku hizi wazazi wengi wapo busy kufuatilia tamthilia, kufikiria marejesho ya Vicoba, na kuperuzi MEMES huko facebook, Tik Tok, na Instagram kupitia smartphone zao. Hawana muda wa kufuatilia nyendo za watoto wao - eti wanatafuta pesa. Je, hizo pesa unamtafutia nani kama mtoto wako anaangamia?
👁️ WAZEE WETU WA ZAMANI:
Wazee wetu wa zamani walituzaa na kutulea vizuri sana. Wengine walizaa watoto zaidi ya 10, na waliweza kuwalea watoto wao licha ya kuwa wazee hao hawakuwa na elimu kubwa wala biashara za super market. Hakika wazee wetu waliweza kutulea vizuri sana - walitusomesha, walitulisha, walituvisha, walitufundisha maadili mema, na walitufuatilia kwa ukaribu sana, kwa kweli wapewe maua yao.
👁️ WAZAZI WA SIKUHIZI:
Wazazi wa siku hizi (sio wote) hawajui kulea watoto wao kabisa, yaani wamevurugwa na pesa. Licha ya wazazi wengine wanamiliki pesa, elimu, magari, nyumba, na biashara lakini hata wakizaa mtoto mmoja wanashindwa kumlea mtoto wao - wazazi wapo busy kuzunguka kwenye kumbi za starehe.
Wazazi wa siku hizi wakirudi nyumbani wapo busy na smartphone au tamthilia, wengine wanawaza Vicoba, hawana utamaduni wa kupekua madaftari wala mabegi ya shule ya watoto wao, wala kuzungumza na watoto wao. Siku hizi watoto wanaandamwa na wimbi la kulawitiwa, kubakwa, na kufanyiwa vitendo vingine vya ukatili - ukiacha wimbi hilo, kuna watoto wengine kwenye mabegi yao wanaficha bangi, condoms, silaha kama kisu, na sindano za kujidunga madawa ya kulevya- Aah! inasikitisha sana, wazazi wapo busy kutafuta pesa.
Pengine watoto baada ya kubakwa wanatishwa na wabakaji kuwa wasiseme au wanafumbwa mdomo kwa kuhongwa pipi, biscuits, sambusa, n.k - Hata hivyo baadhi ya watoto wanaolawitiwa pindi wakirudi majumbani wanakuwa na ujasiri wa kusema kwa wazazi; lakini wazazi wapo busy na tamthilia na smartphone. Bila shaka pamoja na wazazi kutowahoji watoto wao, kuna watoto wengine wanajikaza wanaamua kuongea; "MAMA NAWASHWA HUKU, NAOMBA UNIKAGUE" - mtoto baada ya kuongea hayo maneno anategemea akaguliwe ili afunguke vizuri kuhusu tukio baya alilofanyiwa mtaani lakini jibu atakalopewa na mzazi wake ni; UMEZIDISHA SANA MICHEZO HEBU TOKA HAPA.
👁️ JUKUMU LA KUWALEA WATOTO:
Siku hizi jukumu la kuwalea watoto wetu wazazi tumelikataa; tumewaachia taasisi na idara mbalimbali kama vile Polisi, ustawi wa jamii, na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali watulelee watoto wetu, sisi wazazi tupo busy kutafuta hela - Hii sio sawa kabisa.
BY: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es salaam.
Sept 20, 2024.