Malezi: Adhabu gàni na Wakati gàni unapaswa kumuadhibu Mtoto? Hivi ndivyo utakavyofanya.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,654
61,562
MALEZI: ADHABU GÀNI NA WAKATI GÀNI UNAPASWA KUMUADHIBU MTOTO? HIVI NDIVYO UTAKAVYOFANYA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Sasa umeshakuwa na Familia. Au pengine huna lakini unatarajia Siku za karibuni utakuwa na Familia.
Binadamu wôte waliotimamu wanajua Hakuna Maisha mazuri nje ya familia Kwa Sababu familia ndîo Maisha yenyewe.

Kama Mwanaume, na kama Mwanamke. Kabla ya Kupata Watoto kwèñye familia yenye lazima mhakikishe mnawekana Sawa ninyi Kwa ninyi kama Wazazi watarajiwa ili muwe kitu Kimoja. Hii itawasaidia katika Malezi ya Watoto na uimara, ukuaji na future ya famikia Yenu.

Ni hakika Ndoa au familia inaweza kupoteza muelekeo mara tuu Watoto watakapozaliwa licha ya kuwa mlikuwa mnaishi Vizuri Kabla ya Kupata Watoto. Hii inasababishwa na kutokuwa kitu Kimoja ili kuunda familia.

Familia NI neno lenye maana ya Umoja na mshikamano. Familia humaanisha mfanano na kushirikiana.
Siô kîla Nyumba inafamilia ingawaje huenda wanaishi Baba, mama na Watoto.
Ni kama Taífa siô kîla Watu wanaoishi nchi Moja ni Raia isipokuwa wàpo àmbao siô Raia Wengine wahamiaji haramu, Wengine wawekezaji, Wengine wanauraia Pacha.

Unaweza ukaishi na Mkeo/Mumeo kumbe siô Mumeo/Mkeo na hiyo inamaanisha hamwezi Kutengeneza familia Moja.

Hii utaanza kuona athari baàda ya Watoto kuzaliwa.
Hasa Kwa Wababa.

Baba kama Mfalme au Rais lazima úwe Makini kuteua msaidizi àmbaye mtakuwa kitu Kimoja katika safari Yenu ya Maisha.
Unazaa Watoto alafu mwisho wa Siku unafanyiwa mapinduzi au impeachment unaondolewa kwèñye ufalme na anaingizwa mtawala Mwingine katika Taífa Lako(familia yako).

Watoto ni kama wananchi au Raia àmbao ninyi mtawazaa na kuwaongoza. Kama ninyi siô wamoja inamaana uasi na mapinduzi yatatokea Huko mbeleni.

Mtibeli unamaneno Mengi. Mtibeli usitufundishe Maisha..
Mtibeli wewe hujapata hata Miaka 40 huijui Huna ujualo. Hata familia huenda Mtibeli Huna.

Sawa wewe kama unaona hivyo Mimi sikukatazi Kutumia Akili na mawazo yako uwezavyo. Ni hiyari yako kuendelea kunisikiliza au kuacha Wala sitapungukiwa na kitu na wéwe halikadhalika.

Mtibeli embu Acha maneno mengi, endelea.

Sawa Naendelea;

Mume na Mke mshakuwa kitu Kimoja kihisia, kiroho, kimwili na kiakili hasa mtazamo.
Lazima mkaribiane Kwa UFanano. Msipishane Sana.
Ndîo maana haishauriwi Kuoa au kuolewa na Mtu WA Imani ñyiñgine, Mtu wa tamaduni zingine Ambazo hamfanani.

Zaidi haishauriwi Mtu Kuoa wake wengi Kwa Sababu Hakuna familia ya wake wengi ila Ipo Ndoa ya wake Wengi.
Mwanaume anapooa wake wanne tafsiri Yake anafamilia nne.
Au Tuseme ni Mfalme anayetawala nchi nne. Automatically hao Wanawake hauwezi kuwafanya wafanane na wéwe wôte. Ñdipo migogoro inapoanzia.
Hii ni kimalezi.

MALEZI Kwa Watoto huanza kuwa ya tabu pale àmbapo Baba na Mama hawafanani, siô kitu Kimoja. Kumaanisha hakuna familia Hapo.

MALEZI Kwa Watoto ni kama kunywa uji wa mgonjwa yàani Malezi NI rahisi Sana Kwa Mume na Mke wanaofanana hao huunda familia.

Ugumu wa Malezi siô uchumi.
Ugumu wa Malezi sio ukuaji wa Mtoto.
Ugumu wa Malezi sio magonjwa Kwa Mtoto.
Ugumu wa Malezi ni Baba na Mama kutokuwa kitu Kimoja yaani kushindwa kuunda FAMILIA.

Mtu anapokuambia Malezi ni Magumu Kwa tafsiri ya harakaharaka anamaanisha yeye na mwenza wake hawapo Sawa, hawafanani na siô kitu Kimoja.

Maisha ya Mwanadamu ni rahisi Sana pale kunapokuwa na umoja na ushirikiano au Kwa lugha ya mapenzi tunaita Upendo.

Maelezo hayo yôte niliyoyatoa ningeweza kuyafupisha Kwa sentensi Moja kuwa Kabla hujazaa Watoto hakikisha wewe na mwenza wako mnakuwa kitu Kimoja, mnafanana.

Kisha ninapotoa Somo la adhabu Kwa Mtoto ndîo ninaweza kulieleza ili adhabu hizô ziwe na tija.

ADHABU KWA MTOTO

ADHABU ni Malipo stahiki Kwa Mtu yanayolenga kumuumiza baàda ya kufanya au kusema Jambo fulani Baya Kwa lengo la kukomesha tàbia au Jambo Baya lililofanywa

Katika Malezi ya Watoto kûna Adhabu na Zawadi Ambazo Mtoto lazima awe anapewa ili kumpa Mafunzo.

Kumlea Mtoto siô kumlisha tuu au kumvalisha tuu Bali ni pàmoja na kumuandaa katika Maisha yake ya baadaye.

Zawadi ni Malipo anayopewa Mtu kwaajili ya kumpongeza, Kumtia Moyo, kumhamasisha Kwa tàbia njema aliyoifanya.
Hivyo zawadi ni kama reinforcement na motivation Kwa Mtoto.

Kwa hiyo zawadi Ipo Kwa lengo kuimarisha tàbia Njema iliyofanywa na Mtoto au Mtu.
Wakati adhabu Ipo Kwa lengo la kuuzia, kukomesha na kufifisha tàbia Mbaya.

ADHABU hutolewa Kulingana na Umri, jinsia, uelewa na dhamiri ya mtenda Jambo.

Kûna Aina za Adhabu kama ifuatayo;
1. ADHABU ya Maneno tuu
2. ADHABU ya kumchapa Mtoto au kuumiza Mwili WA Mtoto
3. ADHABU ya kuzuia Haki Fulani za Mtoto Kwa Muda Fulani.

Mtoto àmbaye ni mdogo hafanyi Vitu Kwa dhamiri yàani Kwa kukusudia hivyo Huwezi kumchapa viboko.
Mtoto mdogo namaanisha mtoto chini ya Miaka Kumi.
Wengi waô yàani Asilimia 90 hawafanyi Vitu Kwa dhamiri hivyo hawa hupewa adhabu ndogondogo hasa ya kuonywa Kwa mdomo au kunyimwa Haki Fulani za Umri wake.

Haki hizô hazipaswi kuwa Haki za msingi za Mtoto kama Kula, Kulala, kuvaa,

Haki Ambazo unaweza kuziua Kwa Mtoto Kwa Muda Fulani kama adhabu ni kama kutompa Vitu àmbavyo anavipenda Kwa nyakati hizô mfano anapenda kuchezea mdoli Fulani au anapenda kucheza na wenzake au anapenda kuangalia katuni.
Unamzuia Jambo Hilo Kwa Muda labda Siku tatu huku ukimwambia hiyo ni adhabu kwa kosa fulani alilofanya.

Wajibu wa Mzazi Kwa Mtoto anapotoa Adhabu;
0. Ni vizuri unapotoa adhabu íwe Kwa Makosa àmbayo ulimkataza Mtoto. Usitoe adhabu Kwa kosa àmbalo hukuwahi kumkataza Mtoto.

1. Mpe Mtoto Nafasi ya kujieleza Kwa nini kafanya Kosa àmbalo ulimkataza. Ni Haki ya mkosaji pia kupewa Nafasi kujieleza. Kama anahoja msikilize.
Muulize Kwa nini usimpe adhabu alafu angalia kama anahoja.

2. Mzazi unaowajibu wa kumfundisha na kumuelewesba Mtoto kuhusu Kosa alilofanya na uhakikishe amelielewa Kwa maelezo Sahihi yaliyonyooka Kisha awajibike Kwa adhabu utakayompa.

3. Mzazi unawajibu wa kutoa adhabu ya Haki Kulingana na Umri, jinsia, uelewa na Àkili ya Mtoto.
Usimpe adhabu kûbwa Wala usimpe adhabu ndogo.

4. Mfundishe kuomba Msamaha Ikiwa ni pàmoja na kukubali(kukiri) Kosa na kuandika kuwa hatorudia.

5. Kumpa Pole baada ya Kutumikia adhabu huku ukimwambia asirudie tenà kwani akirudia adhabu itakuwa Kali zaidi na zaidi

6. Mwonyeshe yeye ni Mtoto mzuri unayemuamini na àmbaye hastahili kufanya Makosa kama alilofanya.

7. Usimlinganishe na Mtoto yeyote wa Jirani au yeyote anayemjua. Ila mwambie yeye ndiye Mtoto Bora ambaye Watoto Wengine wanajifunza tàbia Bora Kutoka kwàke.

Ni vizuri pia kumfundisha Mtoto kuwajibika Kwa Makosa aliyoyafanya Ikiwa ni pàmoja na wajibu wa namna Ifuatayo;
1. Kukiri Makosa aliyofanya.
2. Kujieleza Jambo ambalo lilimpelekea kufanya kosa Hilo.
3. Kuomba Msamaha
4. Kufanya adhabu au kushauri ni adhabu gàni apewe lakini Mzazi ndiye atatoa Maamuzi ya mwisho.

Makosa ya dhamiri àmbayo mengi hufanywa na Watoto waliokwisha Balehe ndîo hustahili adhabu ya viboko yàani inayogusa Mwili.
Ikiwa ni pàmoja na adhabu zifuatazo;
1. Adhabu ya kufanya Kazi lakini íwe ilingana na Umri na uwezo wa Mtoto Bila kusahau jinsia.
Mfano, Mtoto wa Kiume kafanya Kosa labda kachelewa kurudi nyumbani íwe Kwa sababu ya kucheza Mpira,
Unamwambia Kîla ikifika jioni Saa Kumi na Moja amwagilie bustani ya Maua au mbogamboga, au asafishe banda la Kuku au mifugo.
Alafu akimaliza akuite na kama haupo akupigie Simu kupitia Simu ya Mama au Mtu yeyote aliyenyumbani.

2. Kumfanyisha mazoezi kama kukimbia lakini siô Kwa kumtesa. Au tayari ushajua hajui Kúpiga danadana Mia Moja unamwambia unampa adhabu ya kujifunza danadana ndàni ya Siku Saba awe anajua Kúpiga danadana Mia Moja. Akishindwa utampa adhabu ya kwenda kulima.

3. Kufanya Usafi wa Nyumba kîla asûbuhi yàani ikifika Saa Kumi na Mbili Kamili asûbuhi Nyumba yôte na uwanja úwe msafi. Kwa Siku Saba.

4. Unamletea kitabu chenye kurasa na maudhui yanayolingana na Umri na jinsia Yake. Kisha mpe Siku kadhaa Kulingana na ukubwa wa kitabu, mwambie utamuuliza maswali Kumi Kutoka kwèñye hicho kitabu ulichompa, kîla Swali ni Sawa na fimbo Moja. Akikosa maswali kuanzia matano utamtandika fimbo za maswali aliyokosa na utampa adhabu ñyiñgine tenà.

5. Mpe adhabu ya kulenga shabaha. Anza Kwa kumpa Siku Saba au Kumi ya kujifunza kulenga shabaha. Kama unauwezo mpeleke Kwa walenga shabaha, au mpe Manati au mshale.
Mwambie baàda ya Siku 10 nitakupa Mawe Kumi ulenge shabaha sehemu nitakayokuambia yenye umbali wa Mita kadhaa labda thelasini. Kîla utakayoshindwa itakuwa ni Kiboko chako. Ukishindwa kuanzia Tano, utatandikwa viboko ulivyoshindwa na nitakupa adhabu tenà.

Hiyo ni Mfano ya adhabu unaweza kubuni adhabu nyingi lakini adhabu utakazobuni sharti zilenge mambo yafuatayo;

1. Kukomesha tàbia mbaya ya Mtoto aliyoifanya.
2. Kumfunza na kumjenga Mtoto kupata ujuzi wa kitu Kingine.
ADHABU isiishie tuu kumchapa tuu Mtoto.

Epuka kumnenea Mtoto maneno Mabaya siô adhabu nzuri.
Ila tàbia mbaya usiitukuze Bali isemee maneno Mabaya.

Taikon Acha nipumzike sasa.
Pole Kwa kusoma àndiko refu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom