Malast Born Nina Jambo Lenu

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
6,497
15,205
Screenshot_20250120_124522_Google.jpg


Malast born tunawapenda lakini huwa mna mambo yenu flani flani ambayo yanaboa sana kwahiyo kaka yenu nimeamua niwachane,na hata kama ni mzee kuliko mimi ila kicheo wewe ni wa mwisho kuzaliwa kwahiyo ni mdogo tu

Ni watu ambao mmedekezwa sana na wazazi wenu kwasababu ya kuwa wa mwisho kuzaliwa basi mlipewa attention sana,huwa mlikuwa mnapata mlichokitaka kwa wakati,na hii imewajenga wengi wenu hata ukubwani mnapenda sana attention,mtu asipokuzingatia unamuona mbaya,acheni hayo mambo maisha yamebadilika sana

Ni watu ambao mna sifa ya kuwa tegemezi baadhi yenu,kwakuwa mlikuwa wa mwisho basi mambo mengi mlikuwa mnapewa au mnayapata tu kiurahisi,na wengi wenu ndio maana mnapenda sana kuwa mario,yani kulelewa na mashangazi ndio zenu,kwakuwa mnakumbuka old good days

Na kwasababu hii ya utegemezi ndio nyinyi ambao kila siku mnalialia kwamba mwanamke anafanya kazi lakini hachangii chochote nyumbani,yani mwanamke asipo hudumia familia mnaumia sana kwakuwa bado mna ile hali ya kupenda kufanyiwa mambo flani flani,haya mambo huwezi mkuta nayo first born hata kidogo

Wengi wenu mnaoa lakini hamjui maana ya kichwa cha familia inamaanisha nini,kichwa cha familia kinasimamia mustakabali mzima wa familia,kuanzia kula yao,vaa yao,na kuishi kwao,sasa iweje utegemee mke afanye majukumu yako,malast born grow up guys. Inatakiwa mwanamke aamue tu kukusaidia lakini sio sheria kuwa ana wajibu huo

Mnapenda sana kununanuna,yaani mlishazoeshwa kudekezwa basi mkiamua kununa mnanua kwakuwa mnajua mtabembelezwa tu,ndio nyie ambao mkiwa kwenye ndoa mnawapa tabu mabinti za watu,jambo dogo tu mnanuna,kweli mtoto wa kiume unamnunia mkeo? Acheni huo ujinga grow up guys

Mnapenda sana starehe nyie last born,kwakuwa wakati huo wazazi walishakuwa na uzoefu wa kutosha wa malezi,wakawa wanawaacha tu na wao kudili na mambo mengine,basi mmejikuta watu ambao mko free sana na mnapenda sana kula bata


Hampo responsible kabisa wengi wenu,kwakuwa wakati mnakuwa mmewakuta dada zenu na kaka zenu,basi hamkujifunza mapema kuwajibika,maana kama ni usafi wa nyumba na mazingira basi ni kaka na dada zenu ndio walikuwa wanawajibika kufanya hivyo,nyie miguu juu hamgusi chochote,matokeo yake leo tuna watu ambao hawana ari ya kuwajibika iwe kwenye familia hata kwenye jamiii,acheni ujinga mbadilike


Wengi wenu hamkui bado yani mna utoto mwingi,hamfanyi mambo kama watu ambao wamekomaa na kujua nini wanachofanya,mnajiona bado ni watoto tu,nyie siku zote mnajiona bado bado tu,kamoni ebu mbadilike maisha yanasonga mbele na mkubali kukua sasa


Wengi wenu wajanja wajanja,matapeli wengi ni malast born,nyie ni watu wa sound sana,yani sijui mnajikuta nani aisee,betting pia ndio msiseme,yani mna hela za kuchezea kwakuwa hampendi kuwajibika all you need is just simple money na maisha mazuri

Nyie ni wabinafsi sana,kuanzia udogoni mlikuwa mnasema mdoli wangu,toy langu,baiskeli yangu,na hata ukubwani mmekuwa hivyo hivyo,huwa mnajipa kipaumbele nyie tu,na ukimkuta last born ndio boss au msimamizi wa shughuli flani basi ataangalia maslahi yake kwanza kabla ya watu wake

Hawa ndio kataa ndoa wakubwa,kwasababu hawapendi kuwajibika,hawako tayar kupambana na changamoto za ndoa,utawasikia ndoa ni uwenda wazimu,ndoa ni utapeli,ndoa ni ukandamizaji,haya yote ni kwasababu hawapo tayar kupambana na changamoto za maisha,mbadilike you must grow up young men

Ni hayo tu!
 
Ngoja niwe wa kwanza.
Mkuu, hizo sifa mbona naona zipo kwa watu wote, kikubwa inategemea na familia, malezi uliyopewa na mzazi au wazazi wako. Kuna watu ni first born na wakati kati huko lakini wanasifa kama hizo tajwa hapo. Mimi ni last born lakini sina huo upuuzi ulioandika hapo juu.
 
Ngoja niwe wa kwanza.
Mkuu, hizo sifa mbona naona zipo kwa watu wote, kikubwa inategemea na familia, malezi uliyopewa na mzazi au wazazi wako. Kuna watu ni first born na wakati kati huko lakini wanasifa kama hizo tajwa hapo. Mimi ni last born lakini sina huo upuuzi ulioandika hapo juu.
Asilimia 90 niliyoandika ni mambo ambayo yamefanyiwa utafiti,lakini kama unavyosema mengine wanashea wasio last born pia
 
Back
Top Bottom