Malaika mikaeli alifanikiwa kuchukua mwili wa Musa shetani alipougombea, ukifa mwili wako utachukuliwa na nani? Amua sasa!!

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,910
32,671
Salaam, shalom!!

MADA hii ni fundisho Kwa wale wasioamini kwamba mtu afapo, mwili wake hupelekwa either Kuzimu au Mbinguni.

Na mwili unaopelekwa kuzimu ni mwili upi? Ni huu wa Damu na nyama?

Jibu ni Rahisi tu,

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI, anaishi ndani ya MWILI.

Na ikiwa mtu ni ROHO, uwe na HAKIKA kuwa, mwili wa nyama ni vazi la Roho, hivyo shetani Huwa Hana habari sana na mwili/ vazi, Hilo vazi Huwa ni nyama ya wachawi, funza nk nk.

Anakufa Musa, shetani anakuja kuchukua mwili wa Musa aupekeke gerezani la kuzimu, hapo hapo Malaika mkuu naye anatokea kuchukua mwili wa Musa aupekeke Mbinguni.

Utaniuliza, Musa alikuwa na utashi wakati mwili wake ukigombaniwa na Malaika Mikael na shetani? Jibu ni ndio, afapo mtu, huona Kila kitu Kwa macho Yale halisi ya ndani, mfano mzuri ni macho ya ndotoni wakati ya MWILI yanapofumba unaonaje!!

Malaika mkuu Mikaeli anafanikiwa kuutwaa mwili wa Musa na kupeleka Mbinguni.

Na kuthibitisha kuwa Musa Yuko Mbinguni, Musa alimtokea Yesu pale mlimani na kuongea naye akimtia moyo, ndipo ujue kuwa Mbinguni hata sasa, WATAKATIFU wapo waliokufa ( Roho iliyo hai ilipotengana na miili ya kuharibika) Kisha wakaingia Mbinguni. Na wapo walioingia kuzimu na wanateswa gereza la muda chini kuzimu.

SOURCE: YUDA (1:9)

Ikiwa ungependa Malaika mkuu Mikaeli apate kibali Cha kukupeleka Mbinguni baada ya MWILI huu kufikia mwisho wa uhai, pumzi itapokata, yaani ukitaka Malaika mkuu Mikaeli auchukue mwili wako Kwa kumshinda shetani ambaye pia anautaka, fuatisha Sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

KARIBUNI 🙏
 
Source:

(Mathew 17:1-13) Ukisoma mistari hiyo juu, utakuwa kuwa,

Musa alimtokea Yesu mlimani akiwa na Elia na wakamtia Moyo.

Ndipo ujue mtu ni ROHO,

Hadi ni WA milele,

Mwili ni wa muda tu, usikudanganye, ni vazi la Roho, Roho ndiye mtu halisi mwenyewe.

Ubarikiwe🙏
 
Mwili wangu naomba uchukuliwe na Lamomy 😎
Mwili huo wa nyama ni geresha tu,

Hauna tofauti na nguo ulizovaa, wewe ukivua vazi la mwili, vazi liitwalo mwili litazikwa, wewe halisi mwili wako wa Roho ulio kama Malaika, utapelekwa kuzimu au Mbinguni.

Amua sasa wapi uende,

Ikiwa ni Mbinguni, mkiri Yesu Kristo kuwa BWANA na MWOKOZI WA MAISHA Yako,

Ikiwa unapenda kwenda kuzimu Kisha jehannum,

Endelea na maisha machafu ya dhambi.
 
Back
Top Bottom