Makundi matatu ya watumiaji wa MADAWA YA KULEVYA na je, mtumiaji anaweza kupona?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
677
1,098
Watanzania wengi wamekuwa wakiumizwa na changamoto za vijana wao kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kujikuta wanapoteza malengo yao ya kimaisha kama vile kupata elimu, kuwa na maisha mazuri, kuwa na familia bora na kujikuta wanaangukia kwenye utegemezi mkubwa badala ya wao kutegemewa.

Nikiwa mshauri na mwandishi mbobezi wa masuala ya dawa za kulevya na uhalifu Afrika nieleze kwa ufupi juu ya changamoto hii.

Matumizi ya dawa za kulevya holela ni kinyume na sheria zetu za Nchi ikiwemo sheria ya dawa za kulevya ya Tanzania.

Dawa za kulevya zina athari ya kimwili, kiroho na kiakiri, athari hizo zote uenda kwa pamoja na haziwezi kukuacha salama kama unatumia dawa za kulevya.

Dawa za kulevya zinawekwa kwenye makundi makubwa matatu:

Madawa.jpg

Kundi la kwanza
Vichangamshi. Kundi ili linajumuisha zile dawa za kulevya zenye kuleta uchangamshi zenye asili ya mmea wa cocaine, hapa tunazungumzia cocaine yenyewe, ambapo mtu anapotumia muda wote atakuwa mchangamfu.

Kundi la pili
Vipumbaza, kundi ili ni aina ya dawa za kulevya zenye kupumbaza, yani mtu anapotumia anakuwa legelege, hapa dawa za kulevya zinazohusika ni heroine. Mtumiaji wa kundi ili anapotumia anakuwa anavaa uhusika wa kuishi kwenye Dunia nyingine na kumfanya kulala muda mwingi na kutafuta faraja za muda.

Kundi la tatu
Maruweruwe, kundi ili linajumuisha dawa za kulevya zenye kuleta hisia mbaya ya ujinamizi kama ndoto mbaya na mambo mengine.

Mfano wa kundi ili ni dawa za kulevya aina ya bangi ambapo mtu akivuta anaweza kuona anakimbizwa na panga na mtu mwingine yote hii inasababishwa na maruweruwe.

Haya ndiyo makundi makubwa matatu ya dawa za kulevya japo yapo mengine madogo madogo ambayo yanaweza kutambuliwa na kuingizwa kwenye makundi haya makubwa, mfano matumizi ya dawa za kutengenezwa kienyeji kama petrol au gundi au matumizi ya kiwango cha juu cha dawa za viwandani.

Kimsingi dawa zote zina athari kubwa kwa afya ya binadamu.

Je, mtu anayetumia dawa za kulevya anaweza kupona?
Jibu ni ndiyo mtu anayetumia dawa za kulevya anaweza kupona kabisa na kuacha kutumia dawa za kulevya kwa kupata huduma kwenye vituo vya sober house, ushauri nasaha au kuhudhuria kliniki maalumu za dawa za kulevya.

Kwenye somo langu la pili nitaeleza kwa kina juu tiba hizo kwa leo niishie hapa kwa kusisitiza kuwa usikate tamaa kama una kijana wako ambaye amedumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya chukua hatua unaweza kumuokoa bila kumnyanyapaa.

Source: Malunde
 
Je Punyeto sio dawa ya kulevya? Na inaingia kundi gani hapo.
 
View attachment 2150144

Salaam,

Kumekwa na ongezeeko kubwa la vijana wetu kuharibikiwa kutokana na utumiaji wa mihadarati na ulevi wa kupindukia. Hii inatokana na changamoto za kimaisha kama vile kuvunjika kwa ndoa wakati wa utotoni, Malezi ya mzazi mmoja, Kufiwa katika umri mdogo, Kunyanyaswa hasa kunyanyaswa kingono, Kushindwa kukabiliana na hisia, kuvamiwa na misukumo ya marafiki na mabadiliko ya kitabia.

Tunatoa huduma ushauri na semina kwa vijana. Endapo wewe ni Mzazi au mlezi, Kiongozi wa dini, Mwalimu, Daktari au muuguzi na unae kijana au unafahamu familia yenye kijana anaetaseka, wa kike na wa kiume basi unaweza kuwasiliana nasi,

AMKA SIMAMA USIONE AIBU HAUKO PEKE YAKO

Karume

Kigamboni Sober House: MRC Tanzania
+255742550551
samsonkarume@gmail.com

Upatapo Ujumbe huu, Share na wengine
 
Kundi la tatu
Maruweruwe, kundi ili linajumuisha dawa za kulevya zenye kuleta hisia mbaya ya ujinamizi kama ndoto mbaya na mambo mengine.

Mfano wa kundi ili ni dawa za kulevya aina ya bangi ambapo mtu akivuta anaweza kuona anakimbizwa na panga na mtu mwingine yote hii inasababishwa na maruweruwe
Hapa umetupiga na kitu kizito kichwani...
Sio kweli kabisaaaaaa...napinga....
Hata scientific desription yake, sio hivi.....
Kajipange upya...
 
Back
Top Bottom