Kumekuwa na mijadala mikubwa ikiendelea nchini sasa kuhusu yale yanayoitwa maridhiano ya kisiasa. Kimsingi ni maridhiano kati ya chama tawala na vyama vya upinzani. Lakini haikupaswa kuwa hivyo tu, wapo watu binafsi, mashirika na makampuni binafsi na hata baadhi ya nchi ambazo kipindi cha utawala wa Magufuli walivurugwa na kusababisha maumivu makubwa. Tanzania ilipoteza sifa yake ya kimataifa kama taifa la haki na amani.
Nayaunga mkono maridhiano yanayoendelea hivi sasa. Rais Samia ameonesha utayari kwa kiasi kikubwa na nina imani yapo mengi sana yatafunguka na hii itaifanya nchi yetu kurudia tena kuwa taifa lenye kuaminika katika medani za haki na amani.
Zaidi sana nawapongeza viongozi wa CHADEMA kwa ufundi mkubwa wa kuongoza na kuleta maridhiano yenye kuleta haki na amani. Wale msiopenda maridhiano ni watu wasioitakia mema nchi yetu na mtabaki kuponda jitihada hizi kwani mlifaidika na dhuluma zilizokuwepo. Hongera Samia, Mbowe na wote wenye mapenzi mema.