Makosa ya kuepuka baada ya mahusiano kuvunjika

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,600
Mahusiano yanapovunjika huwa kuna mabadiliko ambayo hujitokeza ndani ya mwili, Watu wengi hawajui kueleza maumivu hayo husema tu "mapenzi yanauma sana" lakini ukihoji yanauma vipi na sehemu gani wengi hawajui wala hawawezi kueleza.Hivyo basi badala ya kuishi huku unasikia stori za mapenzi yanauma sana.Fahamu hayo maumivu yanayotokana na mahusiano kuvunjika.

MABADILIKO YA MWILI BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA

Mahusiano yanapovunjika iwe baada ya fumanizi, usaliti, kutishiana kuachana, kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kugombana, kupeana kashfa na tuhuma za usaliti,iwe baada ya mwenza wako kusafiri kisha anaamua kukaa kimya muda mrefu sana bila taarifa (ghosting) utaona mabadiliko yafuatayo mwilini.

-Kupata hasira kupitiliza,uchungu mkali sana,kuumia kooni,hisia za kisasi,kumchukia sana Mwenza wako,kutamani kumuua,kutamani kumdhuru,kutamani kumdhalilisha hadharani,kutamani kumpiga sana mwenza wako,kutamani kuharibu haribu mali zake zote.

-Hisia za upweke,hisia za simanzi, majonzi, kizunguzungu, kichefuchefu,kujiona mbaya sana wa muonekano,kujiona mzee sana au kukonda sana, kupoteza hamu ya kula au kula sana vyakula bila mpangilio

-Kuwachukia sana watu wa jinsia tofauti,kutamani kujiua, kutetemeka sana,mwili kuishiwa nguvu, kupoteza hisia kwenye vidole,moyo kwenda mbio,kulala sana mpaka unachoka au kukosa usingizi,

-Kukosoa nguvu za kutoka kitandani,kuona aibu, kujichukia sana, kujilaumu,kutokwa machozi,kuanza kulia sana,hofu ya kuishi mpweke milele,kutokwa jasho bila joto,kuharisha ghafla,kubanwa na choo kubwa na ndogo ghafla,hofu ya kuchekwa,hofu ya kudhalilishwa hadharani.

MAKOSA YA KUEPUKA BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA

-Kuamini hauwezi kuishi bila yeye,
-Kutaka kujenga naye urafiki au kuomba aseme kwanini amekuacha ghafla kwa sababu hawezi kujibu na badala yake maumivu makali sana,upweke uliopitiliza utazidi kuongezeka

-Kujaribu kumsahau haraka huzidisha maumivu makali sana moyoni
-kumchafua kwenye mitandao,huzidisha maumivu makali sana moyoni,upweke huongezeka hasa pale ambapo atakaa kimya au atakuchukulia hatua za kisheria

-Kutafuta mwenza mbadala haraka ili kumuumiza - madhara yake mwenza wako mpya utamchukia sana bila sababu zozote, vilevile mwenza wa zamani kama atakaa kimya bila kuuliza chochote utajiona mpweke kupitiliza

-Kuendeleza mawasiliano husababisha kurejesha matumaini ya kisirisiri kwamba anaweza kubadili mawazo mrudiane lakini kama hataki mrudiane upweke huongezeka

-Kumbembeleza,kuanza kulia, kujilaumu,kutishia kujiua, kutuma sms mfululizo, kupiga simu mfululizo, kutuma pesa kibao ili kumshawishi mrudiane

-Kujisifia sana kwenye mitandao ili kumfanya aone wivu kwamba maisha yako ni mazuri sana kuliko enzi mpo pamoja.Madhara yake upweke utazidi kuongezeka kama haonekani kujali chochote kuhusu post zako za kwenye mitandao.

MAUMIVU YA MAHUSIANO KUVUNJIKA HUONGEZEKA KWA SABABU ZIFUATAZO
-Kuzaa naye watoto kisha watoto wanauliza baba au mama yupo wapi

-Kuona aibu mtaani marafiki zako wakiuliza shemeji yupo wapi

-Kumtegemea kiuchumi

-Kama mwenza wako amekuambukiza ugonjwa usiokuwa na tiba kama ukimwi kisha ametokomea kusikojulikana

-Kama mwenza wako ameuza mali zako zote kisha ametokomea kusikojulikana

-Kama mwenza wako amerudiana na ex wake baada ya wewe kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea, kumsaidia sana kipindi kigumu sana kifedha, kumfariji, kumliwaza, kumtetea alipokuwa ametelekezwa na ujauzito au watoto

-Kama mwenza wako amekuacha ghafla kipindi kigumu sana kifedha lakini ulipokuwa na fedha ulijitoa mhanga kumsaidia yeye na ndugu zake

-Kama umeachana naye baada ya ugomvi mkubwa ikiwemo kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha, kukujibu vibaya, kutishia muachane, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano, kukunyima unyumba,au kukungilia kinguvu -Kama ulipambana kumbadilisha tabia kama vile alikuwa mlevi kupindukia, mcheza kamari, mhalifu, mwizi, msaliti wa mara kwa mara,alikuwa na matumizi mabovu sana ya fedha n.k lakini ulijipa matumaini atakuja kubadilika

-Mwanamke (kama ulijibebesha mimba,au kujitolea mahari, kujitambulisha kwa mama yake mzazi lakini mama yake mzazi alikukataa.
 
Siku hizi sioni wala kuhisi tofauti yeyote mahusiano yakiisha.

Kwa wanaume
-eat healthy
-fanya mazoezi
-invest for future
-don't be simp
-kaa mbali na wake za watu
-Tumia muda mwingi kutafuta mafanikio na sio kutafuta wanawake.
-ukimpata anaekupenda na kukuheshimu do the same.

Kuhusu wanawake wataambiana wenyewe.
 
Siku hizi sioni wala kuhisi tofauti yeyote mahusiano yakiisha.

Kwa wanaume
-eat healthy
-fanya mazoezi
-invest for future
-don't be simp
-kaa mbali na wake za watu
-Tumia muda mwingi kutafuta mafanikio na sio kutafuta wanawake.
-ukimpata anaekupenda na kukuheshimu do the same.

Kuhusu wanawake wataambiana wenyewe.
Real men lie on those points
 
Back
Top Bottom