Makontena ya Makonda yadoda, kugawiwa kwa umma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
IWAPO Makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yanayopigwa mnada na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kupitia Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart yatakosa mnunuzi, yatagaiwa kwenye taasisi za umma.

Leo tarehe 15 Septemba 2018 makontena hayo yalipigwa mnada kwa mara ya nne mfululizo na kukosa wanunuzi, kutokana na wateja waliohudhuria kwenye mnada uliofanyika bandarini jijini Dar es Salaam, kushindwa kufika bei elekezi.

Makontena hayo 20 yenye samani mbalimbali ikiwemo meza na viti vya ofisi, yanapigwa mnada baada ya kukwama bandarini kutokana na kudaiwa kodi ya kiasi cha Sh. 1.2 bilioni. Na kwamba TRA imepanga bei elekezi kwa kila kontena kuwa ni Sh. 60 milioni ili kufidia deni hilo.

Kwa mujibu wa Kamishna wa TRA,Charles Kichere amesema kuwa, bei elekezi ya makontena hayo haitaweza kupungua kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki, kama baadhi ya wateja wanavyopendekeza.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kamishna Kichere ameeleza kuwa, endapo wanunuzi hawatafika bei elekezi, sheria inaelekeza kuwa, makontena hayo yagaiwe kwenye taasisi za umma.

“Bei inapangwa kwa mujibu wa sheria, kabla ya bei kupangwa hesabu hukokotolewa ikiwemo ushuru wa forodha na gharama za kuhifadhi mizigo. Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki inaelekeza jinsi ya kukokotoa bei elekezi,” amesema na kuongeza Kamishna Kichere.

“Bei ya makontena iliyopangwa haiwezi kupunguzwa kwa mujibu wa sheria, na kama yakikosa wateja kuna utaratibu wake unaofuata. Inawezekana yakagaiwa katika taasisi za umma au kwenye huduma za kijamii.”
 
First priority - Walimu
20023542003_hero_listings_large.jpg
 
Naamini mikoa yote itanufaikabna kazi nzuri wa makonda ya kuleta msaada na sasa utagusa watu wengi zaidi
 
Wakikkuambia tatizo na mimi nijulishe maana na mimi ni mhenga
 
Vikigawiwa Na Mikoa Mingine maana yake Kazi ya Bw. Makonda imeanza kuvuka Mipaka ya 'Mkoa wake'

Itathibitisha kuwa Paulo Ni Mkuu wa Wakuu wa Mikoa japo RC
bora anatoka Simiyu
 
Ingekuwa hiyo sheria wanayoing'ang'ania imetoka kwa Mungu sawa tungesema haiwezi kutenguliwa, lakini sheria zenyewe hizi zilizotungwa na akina Musukuma, kwanini hiyo bei isishuke?
 
Hapo kuna jambo linafichwa, Watanzania tuko warahisi kweli kudanganywa. Ukiisha sikia wanagawia ofisi za umma au huduma ya jamii, basi hutaijua "criteria" ya kugawa na hapo ndipo walioagiza watakapochukua mzigo bila kulipa kitu. Hakika hakuna cha kushangaza au kipya. Waliorudisha za Escrow hatujui ni lini, wapi na kiasi gani, Waliorudisha za EPA pia hatujui chochote. Sasa mwananchi atajua hili litaishia wapi? Ahhh!
 
Back
Top Bottom