Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Kama yapo ICD ina maana yamehifadhiwa hayajafichwa!! Waache siasa! Hayo mengine yanaenda nje nchi na hata Ushuru hayajalipiwa! Utasemaje yamefichwa?? Unawezaje kufich kontena kwenye Bandari kavu??
Hapo sasa.....makontena 162 yamefichwa....really?? kwenye bandari kavu??
 
Bandari kavu huwa ni custom bonded warehouse, mfanyabiashara anawezaje kuficha bidhaa humo? Urasimu wa Ku clear imports goods na TRA na vyombo vingine usitupiwe kwa wafanyabiashara kwa misingi ya kutafuta sifa tuu
 
Hapo sasa.....makontena 162 yamefichwa....really?? kwenye bandari kavu??
Hivi hawajui uwepo ('kufichwa') wa hayo makontena kwenye ICD ni gharama kubwa na inaongezeka kadri siku zinavyoongezeka kwa kuwa kuna gharama zzinazotozwa na ICD kwa kuhifadhi hayo makontena?
 
Inaoneka tunaweza kulamba sukari ya nchi jirani zetu halafu ikawa balaa, maana wengine wanaweza wakaidai hata kwa kutumia zana zenye ncha kali.
Nawashauri wawe wanapitia SUDECO na TRA kwanza kabla ya kutangaza ugunduzi wao wa vitu vinavyo julikana kitambo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…