Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,193
- 3,248
Wakuu,
Baada ya kutema cheche siku ya Jumapili, Paul Makonda ameendelea kutoa matamko mbalimbali
Siku ya leo akiwa anaongea na wanahabari, Makonda amesema kuwa kazi ya kuwa kiongozi ni ngumu sana na hata yeye alikuwa anaingiza pesa nyingi akiwa mfanyabiashara kuliko sasa hivi akiwa analipwa mshahara kama Mkuu wa Mkoa
"Imefika hatua viongozi wanatafuta watu wa kuwasifia. Hata mfalme Daudi alikuwa ana watu ambao kazi yao ni kupiga vinubi. Maana yake nini? Maana yake ni kwamba kiongozi anataka asikie mziki apate faraja fulani"
"Kazi ya uongozi ni ngumu. Mimi nilikuwa nafanya biashara. Nilivyotoka kwenye uongozi hapa nilikuwa nafanya biashara nikaanza kutengeneza faida. Nimekuja kwenye uongozi biashara zangu zinaharibika. Hela ninayopata kwenye biashara ina faida kubwa mno kuliko hela ninayopata kama mshahara wa ukuu wa mkoa"
======================================
Huyu mbona anaongea kama analazimishwa? Kama alikuwa anapata faida kwenye biashara kwanini amerudi kwenye siasa? Nani kumlazimisha huyu kuingia kwenye siasa?