LGE2024 Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,366
3,787
Wakuu,

Jiwe limerushwa gizani, wakuu mjitokeze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, na baadaye uchaguzi mkuu, vyote ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

======

Tumeongozwa na Rais Samia Kwenda kujiandikisha ikiwa ni siku ya kwanza yah atua ya mwanzo ya wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kuna daftari linalokutaka wewe ujiandikishe kwenye mtaa wako, Kijiji chako au kitongoji chako ili upate uhalali wa kuchagua viongozi akiwemo Mwenyekiti, na wajumbe wake katika mtaa au Kijiji husika.

Usisubiri kumchagua diwani, mbunge na rais ndio ukaona umeingia kwenye uchaguzi la hasha. Tunavyowachagua wenyeviti wa mitaa na vijiji watu wazuri, waadilifu, wenye ahadi za kweli na wanatekeleza, waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya, watu ambao si sehemu ya majambazi wakapata nafasi hiyo maana yake tayari utaleta chachu katika ngazi ya kata, kwakuwa kwenye kata utakuwa umempa nafasi yule Diwani kupata viongozi wanaoleta hoja za wananchi kwenye baraza la kata, ikiwa ni majengo ya shule, ofisi ya mtendaji wa mtaa, etc yako maeneo yametengwa kwaajili ya kujiandikisha.

Pia soma: Dodoma: Rais Samia ashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Lakini pia kuna maeneo mengine unakuta yana umbali kwenye baadhi ya mitaa wamewekewa zaidi ya vituo vitatu mpaka vitano kutegemeana na ukubwa wa mtaa. Lakini pia hata kwenye vijiji au vitongoji nako ni sehemu moja wapo kama ni ofisi ya mwenyekiti wa mitaa/Kijiji, kama ni kwenye tawi kwa maana kwamba kwa mtendaji wa mtaa kote kule wametoa fursa ya kuweka maeneo ya kujiandikisha na pale ambapo hakuna majengo ya serikali/umma maeneo ya wazi nayo yametengwa kwa kazi maalum na kuwekewa watu watakaohusika kujiandikisha.

Hivyo niwaombe tujitokeze kwa wingi kujiandikisha, Arusha tunasema shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya taifa lako.

 
Back
Top Bottom