Katika majimbo yanayoleta changamoto kubwa kwa CCM nyakati za uchaguzi ni jimbo la Arusha mjini. Kibaya zaidi changamoto kubwa huwa ni ndani ya CCM kwenyewe wakati wa kupata mgombea ubunge kupitia CCM. Kwa utafiti wangu binafsi nadhani CCM Arusha ndo imejaa mamluki wengi sana wa CHADEMA kuliko majimbo mengine. WanaCCM ambao husaidia CHADEMA kisirisiri wapo sana ndani ya CCM Arusha.
Hii hitilafu ndani ya chama husababisha mgombea wa CCM kuwa dhaifu dhidi ya mgombea wa kudumu wa CHADEMA ndugu Godbless Lema. Nimetamka mgombea wa kudumu kwa sababu ndani ya CHADEMA kuna watu ni kama wamiliki wa hizo nafasi za kugombea ubunge. Lema, Heche, Sugu, Wenje, Pumbulu, Mbowe, Msigwa na Mnyika ni wagombea wa kudumu kwenye majimbo yao.
CCM Arusha hadi sasa sijaona kada mwenye nguvu za kisiasa kumkabili mgombea wa kudumu Lema. Mbunge Gambo anamalizia muda wake kwasababu haitawezekana kwa yeye kugombea tena Arusha. Ni mfitini asiyetakiwa hata na CCM Arusha. Meya wa jiji, Max Iranqhe naona naye anapambana kujiweka sawa lakini kiukweli kisiasa bado ni mchanga. Amekaa kiutendaji zaidi. Alberto Msando yuko vizuri kisiasa ila naye anatajwa tajwa kwenye mambo yasiyo mazuri hivyo wapinzani kumbomoa ni rahisi. Mzee Monaban kashapoteza mvuto baada ya kushindwa mara kadhaa. Mwenezi Bananga bado nguvu yake ngazi ya jimbo zima ni ndogo.
Kwa sasa mwenye nguvu kisiasa kuliko mwanasiasa yeyote ndani ya Arusha ni RC Makonda. Mambo yake anayofanya yanamweka karibu sana na wapiga kura. Kama akiendelea hivi hadi 2025 basi CCM impitishe kugombea Arusha mjini.