Makonda kugombea ardhi ni somo kwa Watanzania

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,034
20,371
Makonda kugombea ardhi ni somo kwa Watanzania

Ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuna mnyukano. Ni baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohammed (GSM). Wanagombea ardhi.

Makonda analalamika kuwa GSM anataka kumdhulumu mali yake. Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa akatoa ushahidi wa umiliki wa ardhi yenye mgogoro. Kwamba ni mali halali ya mteja wake.

Nani mmiliki? Hilo jawabu litajulikana mbele ya sheria. Msingi wa makala hii ni kumtazama Makonda anayelalamika kuwa anadhulumiwa na mfanyabiashara aliyemwita tapeli. Hana nguvu!

Ikikupendeza, rudi nyuma miaka mitatu tu. Je, ungedhani yule Makonda, mkuu wa mkoa, angekuwa huyu anayesema yupo tayari kupigwa risasi lakini si kushuhudia mali yake ikichukuliwa?

Yule Makonda tishio, mpaka Serikali ya Marekani ikatoa taarifa ya kumpiga marufuku kukanyaga kwenye taifa hilo, kwa sababu waliyoitaja kwamba ni kudhulumu haki ya watu wengine kuishi, ndio huyu asiye na nguvu zozote?

Makonda yule aliyevamia kituo cha Clouds TV na hakufanywa chochote. Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alipotaka kusimama kidete haki itendeke, akajikuta yeye ndiye anafukuzwa kazi. Ndiye huyu anayelalamika polisi wanatumiwa kumdhulumu mali yake?

Yule Makonda aliyeamuru mfanyabiashara, Yusuf Manji na pesa zake akae ndani na akakaa. Aliyemlaza mahabusu Askofu Josephat Gwajima. Ongeza wafanyabiashara wengine wengi na wasanii. Huyu kawa mlalamikaji.

Makonda aliyeamuru Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, akamatwe na ahojiwe. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alikamatwa barabarani kama jambazi ili akahojiwe kuhusu tuhuma ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Ni kwa amri ya Makonda.

Wapo watu hoja yao ni uwezo wa Makonda kumiliki mali za mabilioni. Na kulilia kabisa. Kwamba kwa mshahara wake, hiyo mali ya thamani ya mabilioni angepataje?

Mimi sipo huko, nauliza; Makonda angeendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, halafu nchi ingekuwa chini ya hayati Dk John Magufuli, GSM wangethubutu kugombea naye ardhi?

Unamzunguzia Makonda aliyekuwa anawaita maofisa waaandamizi wa Wizara ya Ardhi na kuwaweka ndani. Hao, wangewezaje kuthubutu kutamka mali ya Makonda bali GSM? Hapo ndio kwenye shule.

Ruhusa kuelimika

Matokeo ya sasa ya Makonda, kutoka yule ambaye alikuwa hagusiki, akitembea na ulinzi mkubwa, ni shule ambayo kila kiongozi, hasa kijana, anapaswa kutunza akilini.

Uongozi wa kisiasa hupaswi kuuendea kwa pupa. Huja na kuondoka. Ndiyo maana kuna nyakati Makonda yupo mtaani analalamika polisi hawatendi haki. Alipokuwa mkuu wa mkoa, aliwaamrisha atakavyo na wengine aliwalaza mahabusu.

Mambo matatu zingatia kabla hujaanza siasa. Mosi zina tabia ya kujaza upepo, inawezekana ukawa huna uwezo lakini ukawa tishio kwelikweli. Siasa zinaweza kukufanya ujione unakaribiana na Mungu kwa ukubwa. Siasa zinaweza kukupa sifa bora ambazo hustahili, inategemea na jinsi ambavyo upepo umeamua. Kama upepo unakupuliza kwa nguvu, unaweza kuwafanya watu wakuone kwamba hajawahi kutokea mwanasiasa mahiri duniani kama wewe.

Jambo la pili la kuzingatia unapoingia kwenye siasa ni kutambua kuwa siasa huwa na muda maalumu, yaani zina expire date. Unaweza kuwa mwanasiasa tishio mpaka taifa likawa haliwezi kuzungumza siasa bila kukutaja lakini mwisho ukifika utasahaulika kabisa. Usiingie kwenye siasa ukiamini kuwa utakuwa mkubwa kuliko wote kisha utadumu mpaka kifo kitakapokuondoa duniani, utajidanganya. Siasa usiziendee kwa miguu yote miwili, jiwekee akiba ya kuishi pembeni nje ya siasa.

Unaweza kuingia kwenye siasa lakini ukiwa umepishana na upepo, hata ufanye matukio gani utaonekana wa kawaida tu. Wenye upepo wakigusa tu hao wanang’ara, wewe unajiuliza mbona unafanya kazi kubwa na haipewi uzito unaostahili?

Jambo la tatu ni kuwa siasa usiitolee machozi. Ukiadhiriwa kwenye ulingo wa kisiasa fahamu kuwa ndiyo tabia yake. Wenye PhD wengi tu wameshawekwa benchi na wenye elimu ya msingi tu.

Usiumie sana kutochaguliwa, ukahisi kuwa labda hukujenga hoja zenye kueleweka au ulipungukiwa uwezo wa ushawishi. Elewa kuwa wanaosikiliza hoja ni watu na huchagua cha kusikiliza au wanaweza kusikiliza lakini akachagua cha kutunza kichwani. Kuelewa ni utashi.

Na kwa sababu wanaosikiliza kwa utashi wao huamua nani wayapokee maneno yake, ni hapo mtu mwenye kuzungumza pumba anaweza kupigiwa makofi na kuchaguliwa, wewe na pointi zako zote ukakataliwa. Hilo lisikuumize, wanaochagua wana utashi wao.

Ndiyo maana nimesema kuwa usiende kwenye siasa kwa kuingiza miguu yote miwili. Pima upepo kwanza, mguu mmoja utakaouacha nje, utakusaidia kukukwamua upepo wa kisiasa utakapokukataa.

Katika siasa muhimu zaidi chukua hii; Tumia mguu mmoja kupima kwanza kina cha maji baharini, ukishajiridhisha ndiyo ujiachie majini.

Wakati ukionesha umahiri wako wa kuogelea, kumbuka mahali ambapo ulihifadhi nguo zako ufukweni maana baada ya kuogolea utatakiwa kuvaa nguo zikutunzie heshima nje ya bahari.

Tumia mguu mmoja kupima kwanza kina cha maji baharini, ukishajiridhisha ndiyo ujiachie majini.

Wakati ukionesha umahiri wako wa kuogelea, kumbuka mahali ambapo ulihifadhi nguo zako ufukweni maana baada ya kuogolea utatakiwa kuvaa nguo zikutunzie heshima nje ya bahari.
 
nchi nyingi zimesimika vijana katika nyanja za uongozi, na zimefanya vyema kasoro tanzania. Viongozi vijana wamekuwa na walikuwa janga, busara sefuri kabisa.

sehem yeyote ya kutoa maamuzi, ukiona mihemko tambua vijana ndio chanzo. wazee hapa tanzania japo wamepitwa na zama lakn wanasubra kidogo.

makonda sio pekee wa kumlaumu, wapo mapropesa kutoka udsm, kabla ya madaraka walikuwa wakiongea hili, walipopewa madaraka wanaongea lile. unashangaa huyu mtu ana pepo?
 
Kweli vijana wamekuwa tatizo na chanzo kikubwa cha kuharibu (Japo si wote).

Lakini naona wengi wao wanafanya hivyo ili kuwafurahisha walio waweka.

akija kuwa kiongozi tena mtatembelea vidole.usijeze na makonda
Anapigania Mali yake.

Tabia ya wanasiasa (Mliona nilivyopambania Ardhi yangu, ndivyo hivyo nitawapambania)

Wananchi utaskia oyeeeeee!!!!!!
 
Ubabe wa kuchonga una shida sana. Kama wewe ulikuwa na ubabe kwa kutumia nguvu ya dola, wewe siyo mbabe wa kweli. Inaonekana ubabe wa Makonda ulikuwa ni ubabe wa kutumia tuu nguvu ya dola na siyo ubabe wa kweli. Ndiyo maana sasa hivi watoto wa mjini wanamliza.
 
Makonda aliyeamuru Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, akamatwe na ahojiwe. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alikamatwa barabarani kama jambazi ili akahojiwe kuhusu tuhuma ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Ni kwa amri ya Makonda
Makonda aliyewaamuru watu wote wenye silaha kwenda kuhakiki usajili wake na mpaka nambari one naye akaenda kufichua yake na kuihakiki pamoja na ulinzi nambari one aliokuwa nao.
 
Ubabe wa kuchonga una shida sana. Kama wewe ulikuwa na ubabe kwa kutumia nguvu ya dola, wewe siyo mbabe wa kweli. Inaonekana ubabe wa Makonda ulikuwa ni ubabe wa kutumia tuu nguvu ya dola na siyo ubabe wa kweli. Ndiyo maana sasa hivi watoto wa mjini wanamliza.
Yaani hivi vyeo vya muda ni vibaya sana usipotumia vyema.
 
Makonda aliyewaamuru watu wote wenye silaha kwenda kuhakiki usajili wake na mpaka nambari one naye akaenda kufichua yake na kuihakiki pamoja na ulinzi nambari one aliokuwa nao.
Maisha hubadilika sana
 
Makonda kugombea ardhi ni somo kwa Watanzania

Ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuna mnyukano. Ni baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohammed (GSM). Wanagombea ardhi...
DAUDI ALBERT BASHITE anajiabisha kila siku.

Hivi Ana risiti za ununuzi wa hicho kiwanja cha Regent Estate?
Je analipa land rent na tozo nyingine za kiwanja?

Kwanini haweki documents hadharani?

Paul Makonda na jingalao ni kitu kimoja wote CCM.
Chanzo Cha Matatizo
Chama Cha Mazezeta
 
Makonda ni ganda la mua lililoisha utamu lazima ageuzwe. Tajiri gsm hawezi mdhulumu mtu masikini kama makonda. Sema tu sababu ccm inawalinda wahalifu itamkingia kifua lakini makonda ni muhalifu aliyeibiwa wananchi kupitia vitisho vya madaraka kwa maagizo ya jiwe
 
Makonda aliyempiga mkwara hadi Lowasa issue ya watoto wa nje ya ndoa leo analalamika?!kwamba wale waliopotezwa(according to us embassy),waliodhulumiwa nae walistahili ila yeye leo anaonewa?!
 
Makonda ni ganda la mua lililoisha utamu lazima ageuzwe. Tajiri gsm hawezi mdhulumu mtu masikini kama makonda. Sema tu sababu ccm inawalinda wahalifu itamkingia kifua lakini makonda ni muhalifu aliyeibiwa wananchi kupitia vitisho vya madaraka kwa maagizo ya jiwe
Tunaishi na kuishia
 
Dunia inakimbia kwa kasi sana. Yaani kutoka kuwatukana, kuwakejeli maofisa Ardhi mbele ya hadhara kwa kuwaita vilaza/vichaa enzi akiwa RC na Mtoto pendwa wa Magufuli!
Leo eti akienda kwenye hizo ofisi za ardhi kupigania hicho kiwanja inamlazimu kunyenyekea, badala ya kunyenyekewa!

Yule aliyemjaza upepo na kiburi kiasi cha kuoiga simu muda wowote na sehemu yoyote ile, hayupo tena! Nchi sasa imetoka kwenye mikono ya Washamba na Malimbukeni (according to Zitto), na sasa ipo mikononi mwa wenyewe (watoto wa mjini), hivyo ataelewa tu.
 
Ila Mkuu kwa huyu Mtoto wa mjini Ndio kabisa anapiga chenga za mwili.

Ipo Siku mtamuelewa na yeye.
 
Back
Top Bottom