Pre GE2025 Makonda ataibuka aanze kuwananga watesi wake hawamuwezi, Sabaya atalamba teuzi. Tutahamia kwenye ubuyu mwingine, wameshajua ndio tulivyo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,553
4,377
Wakuu wakati tunavuta mashuka nimeona nipite kidogo....

Wenye nchi wameshatujua, tunapenda umbea kuliko hata uhai, wanapiga mziki ule ule ambao tumezoea kuusikia na sisi bila hiyana hao rumba tunalisakata.

Pia soma: Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Sakata la sukari na Bashe jiii, bodi imetoa maelezo ya kipuuzi ndio imeisha hiyo.

Suala la binti wa Yombo, wamekamatwa vijana lakini mafia mwenyewe anafichwa fichwa, taratibuuu tushaanza kuachia.

Suala la watu kupotea hovyo, kariakoo vijana walikuwa wanachukuliwa akipatikana kashafika kwa Sir God, Sativa, Shadrack mpaka sasa hajulikani alipo, TLS imetoa list yake ya watu 83 waliotekwa, taratibu linaenda kuzimika.


Pia soma: Paul Makonda arejea, aibukia Uwanja wa Ndege Arusha uliopo eneo la Kisongo

Tumeletewa vya kutuzuga kwa muda; uteuzi na utenguzi, saivi kila sehemu ni kona ni Ummy na mwenzake aliyechukua nafasi hiyo mishipa ikitusimama kujadili alikotoa mganga wake🤦.

Huku Lissu kapokea mchango toka CCM, ni kutoka kwa wale wale anaowatuhumu kila siku kuwa watesi wao🤦.

Huo ni mwanzo tu, naona kuna bomu linakuja, na safari hii 'mama' atasepa na kijiji. Huku Makonda, kule Ole anarudishwa kwenye mfumo, mpaka tunakuja kushtuka kila kitu kimezikwa. Hao tunarudi kusubiri tuletewe kingine kama mazuzu.

Lini tutazinduka kwenye ujinga huu?
 
Back
Top Bottom