Makonda asimulia Jenerali Mabeyo alivyomuokoa kwenye sakata la makontena

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,752
8,154
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesimulia namna alivyookolewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo katika sakata la makontena ya vifaa vya ofisi za walimu wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna watu walitaka kumchomekea matrekta na magari kwenye makontena hayo.

Makonda aliyasema hayo jana jijini hapa alipokutana na wadau wa mashirika na asasi za kiraia kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Alisema pona yake ni Jenerali Mabeyo kuzuia makontena yasifunguliwe na ulinzi kuendelea kuimarika, la sivyo matrekta na magari yangewekwa katika makontena hayo ili ionekane hakuleta thamani bali ni magari yake.

“Kipindi kile namshukuru Mungu baada ya kugundua taarifa walizozipeleka kwa Rais John Magufuli ni tofauti na uhalisia usiku walitaka kwenda kufungua yale makontena waweke matrekta na magari ili nionekane nilikuwa nadanganya naleta vifaa vya walimu kumbe naleta vya kwangu,” alisema.

Makonda, alisema kulikuwa na wanajeshi wanalinda makinikia ambao wapo chini ya Jenerali Mabeyo walivyowakuta wakaogopa.

“Mabeyo akaweka ngumu hakuna kufunguliwa makontena. Hiyo ilikuwa salama yangu hizi nia njema zina nyakati ngumu sana... halafu huku nimeshatangazwa huyo mkwepa kodi, fisadi anataka kujitafutia mali,”alisema Makonda na kuongeza kuwa:

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa haya mambo ya ufadhili Dar es Salaam nilifanya ile kazi ya ujenzi wa ofisi za nyumba za walimu kwa nguvu kubwa nikaomba wadau wa malori, watu wa vituo vya mafuta wakatoa mafuta, Magereza wakatoa watu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakatoa vifaa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakatupatia askari tukaanza kujenga ofisi za walimu.”

Alisema wakapatikana watu wengine wema kutoka nchini Marekani walijitolea kontena 20 zilizokuwa na thamani. “Zikaingia siasa pale zilikuwa siasa kali kweli kweli, kumbe kuna jamaa wanasema huyu akiendelea hivi na walimu wakimpenda atatusumbua mbele ya safari,”alisema Makonda.

Alisema wakati anapambana kuleta maendeleo kwa walimu wakae katika ofisi nzuri na kuheshimika kumbe kuna baadhi wanawaza tofauti.

“Nilipigwa fitina ambayo sijawahi kuiona duniani ikafika mahali nikasema sasa watajua Mungu yupo ama hayupo. Nikasema hata wakitafuta wateja hawatauza na atakayenunua atalaaniwa yeye na kizazi chake,” alisema.

Makonda, alisema anakumbuka wakati ule bosi wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, aliandika barua na kuelezea msaada huo, ilishindikana na kuendelea kushikiliwa kooni.

“Njemba zimekaa vikao vya usiku wakati huo sikuwa najua yale maombi ya kusambaratisha vikao vya sirini kwa sasa nimeshayajua sasa ninawakung’uta na vikao vyao vya usiku wanavyovifanya,” alisema.

Alisema anaelewa asasi za kiraia zinapata changamoto sio kwa sababu wanaleta vitu kwa ajili ya kuuza bali wengine ni kuoneana wivu.

Alisema kulikuwa na upungufu wa vifaa kwa ofisi za walimu zaidi ya 400 wanakaa chini ya miti, aliomba wadau, hajatumia fedha ya Serikali, mtu mmoja anaungana na mwenzake kuharibu.

“Umoja wa waovu huwa haudumu, wanasambaratika tukikutana wananiambia mheshimiwa vipi nawambia kwa neema nimerudi wewe je? Utasika kwa kweli unatutia moyo sana, tukikutazama,” alisema Makonda.

Alisema kuna mmoja alikutana naye kwenye kahawa akamueleza wao ni wale wa Magufuli wanaonewa. “Nikamuambia acha uongo haukuwa wa Magufuli acha unafiki wewe yaani mtu anataka kutengeneza chuki kama una sifa zako utafanya kazi kama hauna sifa hautafanya kazi,” alisema.
 
1. alete ushahidi asitafute huruma ktk hili mpango alisimamia sheria ipasavyo nadhani alikuwa waziri wa fedha by then..
Thread 'Wewe Makonda, uadilifu umeanza lini? Makontena yako 20 ulikwepa kodi ya sh. 1.2 bilioni. Acha kuhadaa wananchi'
Wewe Makonda, uadilifu umeanza lini? Makontena yako 20 ulikwepa kodi ya sh. 1.2 bilioni. Acha kuhadaa wananchi

2. Hapa Thread 'DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada' DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada
makamu wa rais wakati huo aliwa waziri wa fedha aliamuru yapigwe mnada Je, nae ni kati ya waliokuwa wanamuonea wivu?
Au ndio tabia yake ya kudharau wasaidizi wa rais naye kuwa bingwa w kujikomba kw ofisi kuu?

3. Pamoja na stori yake hyo ya hadaa anataka kusema na rais jpm na alikuwa anania nae mbayaya kumuonea? Soma Thread 'Sakata la Makontena ya Makonda: Rais Magufuli amshukia kama Mwewe, amtaka alipe kodi' Sakata la Makontena ya Makonda: Rais Magufuli amshukia kama Mwewe, amtaka alipe kodi
~ huyu jamaa baste ni bingwa wa had nakujionaa mwema nadhani dr mpano asingekuwepo kwenye nafasi hii makamu wa rais angemshushia tuhu nzito kwamba aliyaka kumuhujumu.

wakubwaa zake wakae nae makimi huyu mfitini na mpenda kujikweza kwa anamaono na uzalendo kuliko yeyote.
 
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesimulia namna alivyookolewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo katika sakata la makontena ya vifaa vya ofisi za walimu wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna watu walitaka kumchomekea matrekta na magari kwenye makontena hayo.

Makonda aliyasema hayo jana jijini hapa alipokutana na wadau wa mashirika na asasi za kiraia kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Alisema pona yake ni Jenerali Mabeyo kuzuia makontena yasifunguliwe na ulinzi kuendelea kuimarika, la sivyo matrekta na magari yangewekwa katika makontena hayo ili ionekane hakuleta thamani bali ni magari yake.

“Kipindi kile namshukuru Mungu baada ya kugundua taarifa walizozipeleka kwa Rais John Magufuli ni tofauti na uhalisia usiku walitaka kwenda kufungua yale makontena waweke matrekta na magari ili nionekane nilikuwa nadanganya naleta vifaa vya walimu kumbe naleta vya kwangu,” alisema.

Makonda, alisema kulikuwa na wanajeshi wanalinda makinikia ambao wapo chini ya Jenerali Mabeyo walivyowakuta wakaogopa.

“Mabeyo akaweka ngumu hakuna kufunguliwa makontena. Hiyo ilikuwa salama yangu hizi nia njema zina nyakati ngumu sana... halafu huku nimeshatangazwa huyo mkwepa kodi, fisadi anataka kujitafutia mali,”alisema Makonda na kuongeza kuwa:

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa haya mambo ya ufadhili Dar es Salaam nilifanya ile kazi ya ujenzi wa ofisi za nyumba za walimu kwa nguvu kubwa nikaomba wadau wa malori, watu wa vituo vya mafuta wakatoa mafuta, Magereza wakatoa watu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakatoa vifaa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakatupatia askari tukaanza kujenga ofisi za walimu.”

Alisema wakapatikana watu wengine wema kutoka nchini Marekani walijitolea kontena 20 zilizokuwa na thamani. “Zikaingia siasa pale zilikuwa siasa kali kweli kweli, kumbe kuna jamaa wanasema huyu akiendelea hivi na walimu wakimpenda atatusumbua mbele ya safari,”alisema Makonda.

Alisema wakati anapambana kuleta maendeleo kwa walimu wakae katika ofisi nzuri na kuheshimika kumbe kuna baadhi wanawaza tofauti.

“Nilipigwa fitina ambayo sijawahi kuiona duniani ikafika mahali nikasema sasa watajua Mungu yupo ama hayupo. Nikasema hata wakitafuta wateja hawatauza na atakayenunua atalaaniwa yeye na kizazi chake,” alisema.

Makonda, alisema anakumbuka wakati ule bosi wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, aliandika barua na kuelezea msaada huo, ilishindikana na kuendelea kushikiliwa kooni.

“Njemba zimekaa vikao vya usiku wakati huo sikuwa najua yale maombi ya kusambaratisha vikao vya sirini kwa sasa nimeshayajua sasa ninawakung’uta na vikao vyao vya usiku wanavyovifanya,” alisema.

Alisema anaelewa asasi za kiraia zinapata changamoto sio kwa sababu wanaleta vitu kwa ajili ya kuuza bali wengine ni kuoneana wivu.

Alisema kulikuwa na upungufu wa vifaa kwa ofisi za walimu zaidi ya 400 wanakaa chini ya miti, aliomba wadau, hajatumia fedha ya Serikali, mtu mmoja anaungana na mwenzake kuharibu.

“Umoja wa waovu huwa haudumu, wanasambaratika tukikutana wananiambia mheshimiwa vipi nawambia kwa neema nimerudi wewe je? Utasika kwa kweli unatutia moyo sana, tukikutazama,” alisema Makonda.

Alisema kuna mmoja alikutana naye kwenye kahawa akamueleza wao ni wale wa Magufuli wanaonewa. “Nikamuambia acha uongo haukuwa wa Magufuli acha unafiki wewe yaani mtu anataka kutengeneza chuki kama una sifa zako utafanya kazi kama hauna sifa hautafanya kazi,” alisema.
Ni wengi tu wamekuzunguka wanajidai walikuwa wa Magu Ili uwasikilize...wananata na biti.
Tanzania hapa kuna watu wabaya sana, wenye fitna na figisu..wenye roho ngumu na mbaya.
Nakushauri Makonda katika Kila ufanyalo sikiliza sauti ya Mungu na ukatende haki. Kuna baadhi ya viongozi ambao ni waonevu na waliumiza watu hapo Arusha, wamekusogelea, wamekuganda na wanajinasibu ni watu wako wa karibu, nakusihi jitenge na uovu wao, wabebe msalaba wao na dhambi zao wenyewe
 
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesimulia namna alivyookolewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo katika sakata la makontena ya vifaa vya ofisi za walimu wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna watu walitaka kumchomekea matrekta na magari kwenye makontena hayo.

Makonda aliyasema hayo jana jijini hapa alipokutana na wadau wa mashirika na asasi za kiraia kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Alisema pona yake ni Jenerali Mabeyo kuzuia makontena yasifunguliwe na ulinzi kuendelea kuimarika, la sivyo matrekta na magari yangewekwa katika makontena hayo ili ionekane hakuleta thamani bali ni magari yake.

“Kipindi kile namshukuru Mungu baada ya kugundua taarifa walizozipeleka kwa Rais John Magufuli ni tofauti na uhalisia usiku walitaka kwenda kufungua yale makontena waweke matrekta na magari ili nionekane nilikuwa nadanganya naleta vifaa vya walimu kumbe naleta vya kwangu,” alisema.

Makonda, alisema kulikuwa na wanajeshi wanalinda makinikia ambao wapo chini ya Jenerali Mabeyo walivyowakuta wakaogopa.

“Mabeyo akaweka ngumu hakuna kufunguliwa makontena. Hiyo ilikuwa salama yangu hizi nia njema zina nyakati ngumu sana... halafu huku nimeshatangazwa huyo mkwepa kodi, fisadi anataka kujitafutia mali,”alisema Makonda na kuongeza kuwa:

“Mimi ni mmoja wa wahanga wa haya mambo ya ufadhili Dar es Salaam nilifanya ile kazi ya ujenzi wa ofisi za nyumba za walimu kwa nguvu kubwa nikaomba wadau wa malori, watu wa vituo vya mafuta wakatoa mafuta, Magereza wakatoa watu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakatoa vifaa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakatupatia askari tukaanza kujenga ofisi za walimu.”

Alisema wakapatikana watu wengine wema kutoka nchini Marekani walijitolea kontena 20 zilizokuwa na thamani. “Zikaingia siasa pale zilikuwa siasa kali kweli kweli, kumbe kuna jamaa wanasema huyu akiendelea hivi na walimu wakimpenda atatusumbua mbele ya safari,”alisema Makonda.

Alisema wakati anapambana kuleta maendeleo kwa walimu wakae katika ofisi nzuri na kuheshimika kumbe kuna baadhi wanawaza tofauti.

“Nilipigwa fitina ambayo sijawahi kuiona duniani ikafika mahali nikasema sasa watajua Mungu yupo ama hayupo. Nikasema hata wakitafuta wateja hawatauza na atakayenunua atalaaniwa yeye na kizazi chake,” alisema.

Makonda, alisema anakumbuka wakati ule bosi wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, aliandika barua na kuelezea msaada huo, ilishindikana na kuendelea kushikiliwa kooni.

“Njemba zimekaa vikao vya usiku wakati huo sikuwa najua yale maombi ya kusambaratisha vikao vya sirini kwa sasa nimeshayajua sasa ninawakung’uta na vikao vyao vya usiku wanavyovifanya,” alisema.

Alisema anaelewa asasi za kiraia zinapata changamoto sio kwa sababu wanaleta vitu kwa ajili ya kuuza bali wengine ni kuoneana wivu.

Alisema kulikuwa na upungufu wa vifaa kwa ofisi za walimu zaidi ya 400 wanakaa chini ya miti, aliomba wadau, hajatumia fedha ya Serikali, mtu mmoja anaungana na mwenzake kuharibu.

“Umoja wa waovu huwa haudumu, wanasambaratika tukikutana wananiambia mheshimiwa vipi nawambia kwa neema nimerudi wewe je? Utasika kwa kweli unatutia moyo sana, tukikutazama,” alisema Makonda.

Alisema kuna mmoja alikutana naye kwenye kahawa akamueleza wao ni wale wa Magufuli wanaonewa. “Nikamuambia acha uongo haukuwa wa Magufuli acha unafiki wewe yaani mtu anataka kutengeneza chuki kama una sifa zako utafanya kazi kama hauna sifa hautafanya kazi,” alisema.
thamani=hapana.
samani=sahihi.
 
Back
Top Bottom