Pre GE2025 ARU Makonda aingia Mtaani usiku Kuuza Uji shamrashamra kuelekea siku ya Wanawake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,956
5,330
Mkoa wa Arusha tayari umeanza shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha siku ya Wanawake duniani kinachotarajiwa kufanyika Machi 08, 2025 kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa na maonesho na shughuli mbalimbali zinazotoa fursa pia kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha kuweza kuuza na kununua bidhaa mbalimbali.

IMG_3300.jpeg

Maclay Company ni kampuni ya Vijana kutoka mkoa wa Arusha ambao wanajishughulisha na mnyororo mzima wa Kilimo, wakilima mazao mbalimbali ya chakula na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo kwa kutengeneza maziwa ya maharage ya soya, Unga wa uji pamoja na viungo vingine mbalimbali kwaajili ya chakula.

Vijana wanaounda kampuni hiyo ni miongoni mwa mamia ya wananchi wa Arusha wanaofanya shughuli zao za kijasiriamali ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid na nje ya viunga vya uwanja huo na leo Februari 28, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
IMG_3301.jpeg

Paul Christian Makonda ametembelea banda lao kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuwafanyia masoko, ambapo kwa muda mfupi alipokuwa kwenye banda lao amefanikiwa kuuza chupa zaidi ya 20 za Uji.
IMG_3303.jpeg
 
Paul Makonda ni Mwamba Kwelikweli huyu Jamaa. Ni chuma hasaa. Yaani ukimuangalia tu unajua kweli huyu ni kiongozi na Mtumishi wa watu.
 
Huyu Jamaa ana maigizo sana..Angekua msanii angepiga sana pesa,ila huku siasani basi tu anawashika wajinga maana zaidi ya usanii hua sioni akifanya mambo yanayolenga kumsaidia mwananchi kabisa.
 
Back
Top Bottom