Makocha kumi bora kuwahi kufundisha mpira wa miguu Tanzania 1990-2022

Championship

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
5,500
10,610
Hawa ndio makocha bora zaidi katika soka letu katika kipindi tajwa hapo juu.

Kigezo kikuu ni idadi ya vikombe ila pia tumeangalia ubora wa mpira na uwezo wa kuboresha vipaji vya wachezaji.

1. James Siang'a
2. Abdallah Kibaden
3. Patrick Phiri
4. Jack Chamangwana
5. Patrick Aussems
6. Syllersaid Mziray
7. Charles Mkwasa
8. Raoul Shungu
9. Stewart Hall
10. Nzoyisaba Tauzany
 
..kocha bora ni Slowmir Work toka Poland aliyeipeleka Taifa Stars kombe la Afrika mwaka 1981.

..kipindi hicho mashindano yalikuwa yanashirikisha timu 8 tu toka bara zima la Afrika.

..Msaidizi wa Slowmir Work alikuwa ni Mtanzania Joel Bendera.

NB.

..pia usijikite kwa makocha wa timu kubwa.

..makocha wanaopaswa kuheshimiwa zaidi ni wale wenye uwezo wa kupandisha timu daraja.
 
Bila Maximo hii list ni takataka kabisa. Wachezaji 70% Wanaocheza kwa kiwango kikubwa hapa Tanzania kwa sasa kwa namna moja au ingine wamepita mikononi mwake.
Hizi ni porojo za vijiweni. Maximo ana mafanikio gani hapa Tanzania? Taja vikombe alivyobeba uache blah blah.

Au taja mchezaji yeyote aliyeibuliwa na kufanywa bora na maximo.
 
..kocha bora ni Slowmir Work toka Poland aliyeipeleka Taifa Stars kombe la Afrika mwaka 1981.

..kipindi hicho mashindano yalikuwa yanashirikisha timu 8 tu toka bara zima la Afrika.

..Msaidizi wa Slowmir Work alikuwa ni Mtanzania Joel Bendera.
Mkuu hapa nimeweka kuanzia 1990 hivyo hao wa huko miaka ya nyuma sikuwataja.
 
Basi tufanye uzi ubatilishwe tuuu
Ubatilishwe kwasababu zipi? Vijana walioanza kufuatilia soka miaka ya 2010s mnataka makocha wa timu zenu ambao wana kikombe kimoja au viwili nao waingie kitu ambacho hakiwezekani.
 
Sasa Unalazimisha!! si ungepost kweny group la ukoo wenu..hapa watu lazima wotoe maoni yao
 
Hizi ni porojo za vijiweni. Maximo ana mafanikio gani hapa Tanzania? Taja vikombe alivyobeba uache blah blah.

Au taja mchezaji yeyote aliyeibuliwa na kufanywa bora na maximo.
Aisee wewe jamaa kumbe ni mweupe kiasi hicho Maximo kaikuta Taifa stars no 137 FIFA rank mpka 97 na tangu aondoke hatuja wahi ingia hata 100 unasema hana kitu?
 
Hizi ni porojo za vijiweni. Maximo ana mafanikio gani hapa Tanzania? Taja vikombe alivyobeba uache blah blah.

Au taja mchezaji yeyote aliyeibuliwa na kufanywa bora na maximo.
Mpaka mwaka 2006, ni vigumu kujua ni Watanzania wangapi walikuwa wamewahi walau kusikia jina la Marcio Maximo - kocha wa soka aliyekuja kuipeleka Tanzania katika fainali za CHAN mwaka 2009. Wachezaji kama Jerry Tegete, Erasto Nyoni, Shaban Nditi ni mkono wake.
 
Sioni ni kwa namna gani kocha wa timu ya taifa atamuibua mchezaji ambaye hafanyi vizuri kwenye klabu yake.
 
Back
Top Bottom