Salaam wana JF,
Ni jamaayangu ambaye ni mtumishi wa umma. Ali share na mimi yanayomsibu. Ushauri zaidi unahitajika tafadhali
Namnukuu kwa ufupi;
''Basic salary yangu January 2016 ilikuwa
937,840/=
Ukiondoa makato yote pamoja na mkopo wa bodi, take home ilikuwa
650,900/=
Nikaona July bajeti mpya mishahara itapanda kidogo japo hata 80 hivyo nikajiongeza kuchukua kamkopo nipate japo kakitalu. Nikawa nabakiwa na
410,300/=. Kwakuwa nilikuwa natimiza majukumu yangu kisawasawa serikalini ndani ya siku3 za kazi, siku mbili nilizitumia kujiongezea kipato
Ghafla bin vuu, mambo yakawa tight.
- Hakuna cha posho wala motisha.
- Chai na lunch ofisini navyo vikayeyuka (kila mtu ajitegemee. Ni maagizo kutoka juu)
- Ni lazima kuripoti ofisini kila siku na muda wa kuondoka una saini
Nikajifariji kuwa mwezi wa saba walau kutakuwa na ahueni. Mara hakuna cha nyongeza.
Akili ikavurugika. Ile nawaza pakutorokea, Bodi wakaja na 15%. Nikaomba uhamisho nikimbilie sehemu ambapo nawezakufanya issue nyingine zakujiongezea kipato walau weekend. Wakati nasubiria majibu ya uhamisho, nikasikia uhamisho umepigwa marufuku.
Take home kwasasa nitabakiwa na
335,400/= Hapo sijagusa hata senti.
Ee Mungu,...kama maamuzi ninayotaka kuyafanya kama ni kwa mapenzi yako na iwe hivyo..ila kama siyo kwa mapenzi yako, niepushie kikombe hiki mie mja wako
''
Mwisho wa kunukuu. Nilichomshauri nikwamba rudi kijijini ukalime au ukafuge. Mshukuru Mungu hujaoa wala huna mtoto