Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,312
152,113
Nakumbuka niliwahi kuleta mada kuhusu nyumba za ibada kufungu vipaza sauti na kusababisha kero kwa wakazi wanaoishi jirani na nyumba hizo na wengi tulitaka vipaza sauti hivi vidhibitiwe kuondoa kero ya kelele

Leo gazeti la Uhuru linaongozwa na habari inayosomeka: "Makanisa ya Kilokole kudhibitiwa mitaani",ni kwa kuimba wakati wa usiku.Hili ni tamko la Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Tunaishauri serikali zoezi hili liwe kwa nchi nzima na liisiishie kwenye Makanisa tu bali hata Misikiti ambayo nayo inayofunga vipaza sauti kwa nje na kusabisha kero ya kelele kwa wanaoishi jirani na Misikiti hiyo wakati wa ibada.



==================

Update;

=================

Baada ya mkuu wa mkoa wa arusha kusema kuwa makanisa ya walokole yadhibitiwe kwa kuwa wanapiga kelele (Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa)

Gwajima ameamua kumjibu mkuu huyo.
https://www.jamiiforums.com/attachments/aud-20160412-wa0001-mp3.337290/
 
Wasipokuwa waangalifu watazua ya kuzua kidini....
 
Mkuu hili ni jambo linalohitaji busara za hali ya Juu, wanaweza kuepusha vipaza sauti lakini bado watu wakaabudu na kuimba kwa sauti za hali ya Juu. Sasa je,tutawapunguza size za midomo yao?

Pili,haitainekana vyema endapo bar na kumbi za starehe zikiachwa hivi hivi huku makanisa na misikiti ikipigwa marufuku kwa kelele za kumtukuza Mwenyenzi Mungu.

Tatu,Serikali iangalie mbali sana katika kulifanya vyema jambo hili. Itaonekana ni uonevu endapo dini moja litapigwa marufuku kuendesha shughuli zao kwa sauti za juu huku nyingine zikiachwa tu zuendelee kama zinavyojitakia.
TAFAKARI.
 
kwani ni lazima serikali ikifanya jambo fulani kwa Watu wa imani fulani lazima ibalance ndo ujisikie sawa?, kama unataka hivyo basi washauri watawala wawe wanateua na waislamu kwa wingi kama wanavyoteuliwa wakiristo katika nafasi za maamuzi nchini.
Nimepost hapo juu kuwa wasipokuwa waangalifu watazua ya kuzua kidini KWA SABABU TUNA WATU WENYE FIKRA HASI KAMA WEWE...
 
Hata mimi nashangaa sana, baa zinapiga kelele kuliko hata makanisa na misikiti.
Nasema yafungwe bar zinafungwa saanne usuiku makanisa mpaka asubuhi bado watu wanalia na kuimba watoti wetu hawawez kujisomea na wagonjwa wanashindwa kupumzika ,na makanisa mwisho wa mkesha iwe saanne usiku
 
Labda ni bora wachangiaji wa mada hii wakaacha kutanguliza hisia za dini zao. Uamuzi wa RC Arusha ni kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) na kanuni zake zilizotoka mwaka jana. Anayetaka kuhubiri mitaani anawajibika kuwa na sound-proof facility/ukumbi kusudi mahubiri yake (ya kiislam au kikristo) yasibughudhi watu wengine. Kwa kimombo NEMA inadhibiti sound polution!
 
Soon devil's worshippers watajidhiirisha hadharani
Devil worshippers ni wale wanajidai kukesha huku wanaimba kwa nguvu na na kelele nyingi ili wasikike ,kama mafarisayo ,kumuabudu mungu sio mpaka ufunge vipaza sauti ...unaweza kuingia ndan ya chumba cha siri umuombe Mungu wako naye atakujazi...kipindi vha yesu watu kama hao aliwapinga ,wanao kaa njii za makutano wakisali kwa nguvu ili wasikike
 
Hapa mtaani kwetu tunajitahidi tu kuwavumilia lakini asiwaambie mtu-- kama issue ni kelele basi ni bora uishi jirani na baa kuliko makanisa ya Walokole! Hapa kwetu kwa mfano... kila wiki wanakesha cku tatu... cna haja ya kuwakumbusha sauti za vinanda vyao! Ikifika Jumapili, ni kuanzia asubuhi hadi jioni-- yaani kitu kinachoitwa kupumzika weekend hakipo kabisa! Narudia, bora uishi jirani na baa!
 
Kuna watu hawajui uchafuzi wa mazingira ni nini...
 
kwani ni lazima serikali ikifanya jambo fulani kwa Watu wa imani fulani lazima ibalance ndo ujisikie sawa?, kama unataka hivyo basi washauri watawala wawe wanateua na waislamu kwa wingi kama wanavyoteuliwa wakiristo katika nafasi za maamuzi nchini.
Dhambi mbaya sana hii inalitafuna taifa. Jiondoe kwenye mkumbo huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…