Nakala zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha kuwa Makamu wa Rais nchini Kenya William Ruto, anashtakiwa kwa kushindwa kuchangia malezi ya mtoto
Nakala hizo zinasema kuwa Bwana Ruto ameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake kama mzazi, wakati mlalamishi ambaye ni mamake mtoto akidai ana haki ya kupata malezi kwa kuwa yeye hana uwezo wa kumlea
Hata hivyo Ruto aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema mtoto wake wa umri wa miaka 11 anatuzwa vyema akiwataka watu wengine wakome kuingilia mambo hayo.