Makamu wa Rais Mama Samia, amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa wakuu wa nchi za SADC

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,459


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Aidha, Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane Swaziland, Makamu wa Rais amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.

Samia Suluhu Hassan amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.

Vile vile, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.

Katika Mkutano huo utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.

Hata hivyo, Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali

Chanzo: Dar24
 
Moja ya muungano ambao Mimi nauonaga haujawahi kuwa na faida kwa Tanzania, South Africa ndio wanaonufaika nao
 
Hongera sana mama Samoa..chapa kazi mpaka wabaki wamesimama wima bila kuelewa Nini cha kufanya.

Pia Ni jambo njema kutoa taarifa hiyo nzuri kwa Taifa na.napenda maendeleo wa nchi hii ..ila tu rekebisha heading mkuu hakuna mkuu wa nchi hapa Tanzanka anayeitwa "Rais Magufulini" ...najua umepitiwa tu na TYPO.
 
Huyu mama bado anamaisha marefu..anaweza akawa mtu muhimu sana duniani hapo badae. Yuko vizuri .

Awamu ya tano hakuna longolongo..Tufanyieni kazi watanzania.
 
Mwisho wa siku nchi za nje zitajua ndio Raisi wa Tanzania!! Ila hafadhali kwa kuwa atatujengea reputation nzuri!!!! Yule mwingine yule sijui hata kama table manner za kwa wenzetu zinapanda !!!! Kule ni lugha tu sio maneno kibao ya kiswahili halafu mwishoni unamlizia na I wish I kud be..... Hawatakuelewa hata kidogo wanataka Porpcorn zipasuke
 
Ras Simba katumbuliwa baada ya kumwambia kuwa hawezi hiyo lugha labda akazaliwe upya uingereza
 
hivi kwenye mikutano ya nje ya kimataifa kama hii huwa anaenda na mumewe.
Vipi protokali imekaaje apo mwenye ujuzi wa protokali ebu atujuze apo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…