Tetesi: Makampuni ya simu kutoa GB 10 kama kufidia hasara na kuomba radhi kwa watumiaji wa mitandao ya simu

Kitombise

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
8,530
25,492
Nyepesi nyepesi;
Nimepata taarifa kuwa jana jumatatu makampuni yote ya simu yanayotoa huduma hapa nchini kuwa wamekaa na kujadili jinsi ya kutatua changamoto na kufidia hasara kwa watumiaji wa mtandao.

Hivyo wamekubaliana kutoa GB 10 kwa kila mtumiaji wa mtandao kama kufidia hasara za bundle walizokutana nazo.

Hizo fidia za bundle zitaanza baada ya huduma kurekebishwa, wamesema ndani ya wiki hii tatizo litakuwa limeisha.

Kila laini itapata GB 10, hata kama una laini 5 basi ukijumlisha utakuwa na GB 50.

Wekeni simu zenu chaji, neema inakuja.

Pia soma>> Watanzania wamefungiwa internet
 
Back
Top Bottom