Makamanda Watano wa CHADEMA wapata nafasi ya kwenda kusoma Nchini Ujerumani

Jesca hon

Member
Jan 9, 2019
8
59
Hizi siasa za Tanzania hazina usawatukiwi tumelala kumbe kuna Makamanda wezetu wanapata michongo kama hii;

Salaam kamanda Yerricko Nyerere,

1. Nakutaarifu kuwa wewe pamoja na makamanda wenzako wanne (4) ambao ni:-

I. Zuberi Mzava

Ii. Noel Shayo

Iii. Aminata Saguti

Iv. Irene Raphel

Mnatakiwa kusafiri kwenda nchini ujerumani kujifunza masuala ya tehama kwa ajili ya kujipanga kukisaidia chama chetu kuingia madarakani 2025, kama ilivyoamuliwa na kikao cha tarehe 17/01/2022 kilichofanyika kwa njia ya mtandao wa zoom.

2. Fedha za matumizi na gharama zote za usafiri na mambo mengine kwa muda wote mtakao kuwa ujerumani zitatolewa na chama cha cdu (christian democratic union) cha ujerumani. Cdu ni wafadhili wetu wa muda mrefu ambao wamekuwa wakitufadhili bila kuchoka, wanapambana kuhakikisha chadema tunaingia madarakani.

3. Utaratibu wa safari ni kwamba tarehe 03.02.2022 mchana mtaondoka nchini, mkitokea nyerere international airport dar es salaam kwenda misri na baadae mtapata conection ya kwenda ujerumani.

4. Tumewasiliana na mwenyekiti freeman mbowe anawatakia safari njema amesisitiza tuwaambie mkawe na mahusiano mazuri na wafadhili wetu cdu. Kwamba mwenendo wenu mzuri utaendelea kuwezesha wafadhili hao kuendelea kutufadhili katika harakati zetu za kuchukua dola. Pia amekuteua wewe kuwa kiongozi wa wenzako.

5. Aidha, mwenyekiti mbowe amesisitiza mkachukue tahadhari zote za kujikinga dhidi ya covid-19. Kwamba muwe makini kwani nchi ya ujerumani licha ya wananchi wake wengi kupata chanjo bado ina idadi kubwa ya maambukizi ya covid-19 ukilinganisha na nchi yetu.

6. Tumekubaliana, mkiwa huko, njia kuu ya mawasiliano iwe kupitia whatsapp na emeil. Wewe ukiwa kama kiongozi utakuwa na jukumu la kutujulisha tabia na mwenendo wa wenzako.

7. Watumie wenzako wote ujumbe huu. Msisitizo mkubwa ni kuwa na nidhamu katika kipindi chote mtakachokuwa kwenye nchi ya watu.

Kutoka kwa

Mratibu wa safari kamanda wilson mwakalukwa
 
Mtoa hoja acha unafiki,watoto wa chama dola wanaposomeshwa nje kwa kodi zetu na kurudi hapa nchini kuendeleza status quo ya kiutawala hii kwako sio habari,wewe sio msemaji wa CDM na elewa kama ni kweli hii taarifa gharama zote hazitagusa kodi yangu au yako,relax na jitahidi kuongelea ukweli na upendo sio uzandiki huu.
 
Wale wa kile chama kingine wakipelekwa nje ya nchi ujue wanaenda kufundishwa namna ya kumaliza watu.

Naongelea chama tawala Cha huku Cuba nilipo.,kwa kina Fidel Castro.
Umesahau na kudukuwa simu za wenzao sababu za uwoga uwoga hawaaminiani wenyewe kwa wenyewe,wako ka tumbili
 
Kwa mfano wakisoma wakamaliza alafu baada tu ya kurudi tz wakaunga mkono juhudi,nini kitatokea?
Nauliza tu ndugu zangu siasa za bongo zinajulikana.
 
Tetesi: Makamanda Watano wa CHADEMA wapata Mchogo wa kwenda kusoma Nchini Ujerumani​

Mchogo ndio kitu gani?
 
Hii mbona imekaa kisanii sanii? Unafadhiliwa na CDU ya Ujerumani lakini unaenda kukaa kwanza Misri? Naona kama kuna mtu anataka kutia fitna.

Amandla...
 
..Ujerumani pia inasaidia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

1642951925831.png
 
Hii mbona imekaa kisanii sanii? Unafadhiliwa na CDU ya Ujerumani lakini unaenda kukaa kwanza Misri? Naona kama kuna mtu anataka kutia fitna.

Amandla...
Ni kawaida kuunganisha ndege, inawezekana hao jamaa hawajapata ndege ya moja kwa moja kwenda Ujerumani.
 
Hizi siasa za Tanzania hazina usawatukiwi tumelala kumbe kuna Makamanda wezetu wanapata michongo kama hii;

Salaam kamanda Yerricko Nyerere,

1. Nakutaarifu kuwa wewe pamoja na makamanda wenzako wanne (4) ambao ni:-

I. Zuberi Mzava

Ii. Noel Shayo

Iii. Aminata Saguti

Iv. Irene Raphel

Mnatakiwa kusafiri kwenda nchini ujerumani kujifunza masuala ya tehama kwa ajili ya kujipanga kukisaidia chama chetu kuingia madarakani 2025, kama ilivyoamuliwa na kikao cha tarehe 17/01/2022 kilichofanyika kwa njia ya mtandao wa zoom.

2. Fedha za matumizi na gharama zote za usafiri na mambo mengine kwa muda wote mtakao kuwa ujerumani zitatolewa na chama cha cdu (christian democratic union) cha ujerumani. Cdu ni wafadhili wetu wa muda mrefu ambao wamekuwa wakitufadhili bila kuchoka, wanapambana kuhakikisha chadema tunaingia madarakani.

3. Utaratibu wa safari ni kwamba tarehe 03.02.2022 mchana mtaondoka nchini, mkitokea nyerere international airport dar es salaam kwenda misri na baadae mtapata conection ya kwenda ujerumani.

4. Tumewasiliana na mwenyekiti freeman mbowe anawatakia safari njema amesisitiza tuwaambie mkawe na mahusiano mazuri na wafadhili wetu cdu. Kwamba mwenendo wenu mzuri utaendelea kuwezesha wafadhili hao kuendelea kutufadhili katika harakati zetu za kuchukua dola. Pia amekuteua wewe kuwa kiongozi wa wenzako.

5. Aidha, mwenyekiti mbowe amesisitiza mkachukue tahadhari zote za kujikinga dhidi ya covid-19. Kwamba muwe makini kwani nchi ya ujerumani licha ya wananchi wake wengi kupata chanjo bado ina idadi kubwa ya maambukizi ya covid-19 ukilinganisha na nchi yetu.

6. Tumekubaliana, mkiwa huko, njia kuu ya mawasiliano iwe kupitia whatsapp na emeil. Wewe ukiwa kama kiongozi utakuwa na jukumu la kutujulisha tabia na mwenendo wa wenzako.

7. Watumie wenzako wote ujumbe huu. Msisitizo mkubwa ni kuwa na nidhamu katika kipindi chote mtakachokuwa kwenye nchi ya watu.

Kutoka kwa

Mratibu wa safari kamanda wilson mwakalukwa

Kuna watu watakuja kusema hiki chama kina ukabila, eti kwann waliochaguliwa kwenda masomoni wengi ni kabila pendwa la Mwenyekiti

Eti Mzava, Shayo na huyu Irene ni wa kabila pendwa la Mwenyekiti
 
Back
Top Bottom