peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,946
Akizungumza leo Aprili 20 hapa Songea mkoani Ruvuma, Makalla amewataka wana CCM kuhamasisha Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu kuchukua mikopo ya halmashauri kujikwamua kiuchumi, na kuachana na mambo ya kuandamana.
"Msingi wa CCM ni katika mabalozi na matawi na CCM tunaamini mkoa wa Ruvuma ni ngome imara ya CCM na hili mtaliendeleza."
"Rais Samia kila mahali katika taifa letu ameweka alama ya maendeleo ndio maana wana CCM wote kwa pamoja tumeridhia katika kuelekea uchaguzi mwakani 2025 nafasi zote zitakuwa wazi kasoro moja ya Urais ambayo CCM tumejiridhisha kwa pamoja kuwa mgombea ni Dk. Samia Suluhu Hassan"
"Hapa mkoani Ruvuma zimetumika Sh bilioni 37 kuboresha uwanja wa ndege wa hapa Ruvuma, hiyo yote ni dhamira ya Rais Samia katika kuboresha sekta ya usafiri wa anga."
"Sh bilioni 2.1 zimetengewa hapa mkoani Ruvuma kwaajili ya mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, wakati wenzetu wanahamasisha maandamano sisi tuhamasishe watu kupata mikopo ya kujikwamua kiuchumi."