LGE2024 Makalla: CCM hatuhitaji upendeleo wala kubebwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, TAMISEMI itende haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,477
4,197

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

CPA Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.

ASKOFU ATATIZWA SABABU ZA KUTEULIWA WAGOMBEA WA CCM NA KUENGULIWA KWA WAGOMBEA WA CHADEMA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Ndugu Watanzania!
Tumeletewa malalamiko yafuatayo kuhusu uteuzi wa majina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika Mtaa wa Stop Over (Kimara), Kata ya Saranga katika Manisapaa ya Ubungo yaliyobandikwa muda mfupi uliopita:

1. Alex Fabian Msuka aliomba kuwa Mgombea kupitia CCM na ameteuliwa kuwa Mgombea. Kwa mujibu wa Fomu yake, aliandika kuwa ni MFANYABIASHARA.

2. Godfrey Benedictor Missana aliomba kuwa Mgombea kupitia CHADEMA lakini hajateuliwa. Kwa mujibu wa Fomu yake, aliandika kuwa ni MJASILIAMALI

Sababu iliyotolewa ya kutokuteuliwa kwake ni kuwa ndugu Missana hajaainisha shughuli maalum anazozifanya kutokana na Kanuni ya 15 (D). Ushahidi wa hayo umeainishwa katika fomu za wahusika, Missana na Msuka.

Je, kuna tofauti gani kati ya mfanyabiashara na mjasiliamali? Je, mtu kuandika mfanyabiashara bila ya kuainisha aina ya biashara anayofanya; na mtu kuandika mjasiliamali bila ya kuainisha aina ya ujasiliamali anaoufanya kuna tofauti?

Je, unafikiri ya kuwa Missana wa CHADEMA ameenguliwa kihalali na Msuka wa CCM ameteuliwa kihalali? Je, unafikiri kuwa haya ni mazingira yanayoashiria Uchaguzi huru na wa haki? Je, kama katika mambo yaliyo wazi kama hili yanazua tafsiri tata na kutokea kutokutenda haki, inakuwaje katika zoezi la kuhesabu kura ambalo litakugubikwa na usiri mkubwa?

Kufuatia hili, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa mamlaka ya juu kuangazia suala hili la Mtaa wa Stop Over. Kama ikionekana kuwa Missana ameenguliwa kwa hila arudishwe na hao waliomuengua waondolewe katika zoezi la kusimamia Uchaguzi huu katika Mtaa wa Stop Over. Na kuwa hii ifanyike pia mahali pengine kote ambako itaonekana hujuma kama hii pia imefanywa kwa makusudi.

Sisi ni sauti ya dhamiri katika Uchaguzi huu na hivyo tunao wajibu tuliopewa na dhamiri kuu ili kihakikisha kuwa sauti ya haki haikauki katika taifa letu na dhamiri iliyo kuu hainyauki kabisa!
Je, kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 8 Novemba 2024; saa 8:00 alasiri
 
View attachment 3147115

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
Mbinu za CCM ni za kijinga sn
 
Nchi ina usengerema mwingi sana hii

Sometimes inatia kinyaa kuona watu wazima wanaongea ujinga
 
View attachment 3147115

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
Shida ni pale unapoongea ambacho humaanishi. Kama kweli unataka ushindane na uonekane umeshinda kwanini umfanyie faulu mpinzani wako halafu useme unapendwa.
 
Amos Makala na chama dola kongwe acheni kuchezea amani ya taifa letu.

7 November 2024
Lisbon, Portugal

HALMASHAURI KUU YA CHAMA (NEC) DOLA KONGWE FRELIMO YAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

Msumbiji: Frelimo inaunganisha maandamano ya baada ya uchaguzi na jaribio la mapinduzi na maslahi ya nje - Tazama​

6:17 | 07 Nov 2024

Frelimosp.yt_

Picha : TVM . Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama (NEC ) dola kongwe FRELIMO katibu wa Siasa na Uenezi Bi. Alcinda Abreu

Chama cha Frelimo kinasema kuwa kuna vuguvugu la kuviondoa madarakani vyama vilivyokomboa baadhi ya nchi katika bara la Afrika kupitia mapinduzi ya kijeshi na kwamba huenda ikawa hivyo nchini Msumbiji.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, chama tawala kongwe FRELIMO kilifahamisha kuwa kinaamini kuwa nchi hiyo ina maliasili ambazo baadhi ya nchi zinatamani
Ilikuwa ni kuwaomba raia wa Msumbiji kuheshimu Katiba ya Jamhuri na kutoa wito kwa wakazi kuwa na utulivu kupitia taarifa kwa umma toka Kamati ya Kisiasa ya Frelimo iliitisha mkutano na waandishi wa habari Jumatano jioni, katika jiji la Maputo.

Bi. Alcinda de Abreu, anayewakilisha Halmashauri Kuu ya chama hicho FRELIMO , aliwasilisha msimamo wa Frelimo kuhusu maandamano na uharibifu katika kupinga uchaguzi mkuu wa tarehe 9 Oktoba 2024.

"Msumbiji, nchi yetu nzuri na tunayopenda, inadhulumiwa kwa njia isiyo ya kawaida, inayoonyeshwa na maandamano ya vurugu ambayo yanaleta maombolezo, maumivu, uharibifu, na kuongezeka kwa njaa na umaskini ndani ya familia kubwa ya Msumbiji," alisema Alcinda de Abreu, anaripoti mwandishi wa shirika la habari la ABNA.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Kisiasa ya chama kongwe dola Frelimo,
"Imechukua miaka ya kazi ngumu kufikia hapa tulipo leo. Tunaelewa kuwa tumepitia nyakati ngumu za mizozo ya kiuchumi na kifedha, iliyosababishwa na sababu za ndani na nje, pamoja na ugaidi huko Cabo Delgado, lakini, kama raia wa Msumbiji, lazima tufanye kazi kwa maendeleo ya nchi, "alisema Bi. Alconda Abreu MNEC mjumbe wa NEC FRELIMO .

Msemaji wa kikao cha 36 cha kawaida cha halmashauri kuu ya chama cha Frelimo alisisitiza wazo la Waziri wa Ulinzi kwamba kuna watu wanaotaka kufanya mapinduzi.

"Frelimo, kama chama kilichoikomboa Msumbiji kutoka kwa ukoloni mkongwe wa Mreno , ni sehemu ya vuguvugu la ukombozi wa taifa, na leo kuna harakati za kuondoa vyama vilivyokomboa baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika ."

MNEC Alcinda de Abreu pia alisema kuwa nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa maliasili ambazo baadhi ya nchi zinatamani na, kwa hivyo, huajiri watu "waliokengeushwa" ili kuchochea ukosefu wa utulivu nchini.
 
View attachment 3147115

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
Shetani akizeeka sana anakuwa malaika ila Kwa kuzuga wajinga TU!
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha Sagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika November 27 mwaka huu, wapo Wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba Wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yanalenga kuwahadaa Watanzania.

CPA Makalla amesema hayo wakati akiongea na Viongozi na Wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam leo November 08,2024, ambapo amesema CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.

“Nitume nafasi hii kuwaomba TAMISEMI ambao ndio Wasimamizi wa Uchaguzi huu, waitendee haki CCM na vyama vingine vyote vitendewe haki, tunaamini Uchaguzi utakuwa huru na haki na atakayeshinda kwa haki, atangazwel

“CCM hatuhitaji upendeleo, hatuhitaji kubebwa, tuko tayari kwani tulishajipanga, hatuhitaji mbereko na TAMISEMI itende haki kwa vyama vyote vya sisasa vilivyoweka Wagombea na sisi tupo tayari kushindana na tutashinda kwa haki”
 
View attachment 3147115

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
Kinachosemwa mbele ya Kamera sichonkinachofanyika nyuma ya camera, na wanalijua Hilo kabisa.
Hakuna yeyote abayeweza kwenda kinyume na maelekezo ya chama katika uchaguzi. Dalili zilikua wazi hasa katika zoezi la uandikishaji.

Kama Ccm inaamini kwamba ujasiriamali sio shughuli maalumu ya kujipatia kipato, huku ilihimiza watu wajiajiri Kila wakati ni dalili makini za mpango wa kujimilikisha madaraka.
 
Walimu walikuwa wanashurutishwa na AROs kuandika majina hewa ccm hivi mnaenda kanisani na miskitini kufanya nini?
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi

Katibu wa NEC wa siasa na Uenezi FRELIMO - kuna njama za kupindua serikali

View: https://m.youtube.com/watch?v=vMH2Lph_8EI
Alcinda Abreu akiongea kuhusu maandamano ya kupinga ushindi wa FRELIMO katika uchaguzi wa Oktoba 9, 2024 ni jaribio la kuangusha ...wapinzani wanaelewa ukweli nani alishinda.

Matumizi ya ghasia kutaka kuvamia majengo ya serikali na fujo zingine ni njia za walioshindwa uchaguzi kutaka nchi isiwe na amani alisema Kamisaa huyo wa Siasa wa chama kongwe dola FRELIMO Bi. Alcinda Abreu akiongea kwa hisia na machozi yakimlengalega huku sauti ikionesha ameingiwa na taharuki kubwa kwa kinachoendelea nchini humo kwa sasa ...
 
Maandamano mjini Beira kufuatia uchafuzi wa uchaguzi uliofanywa na chama dola kongwe FRELIMO kwa kushirikiana na watendaji wa uchaguzi wa serikali ya chama dola Msumbiji
1731082495132.jpeg
 
View attachment 3147115

Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa TAMISEMI kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, wapo wagombea wa CCM ambao wamewekewa pingamizi, hivyo madai ya vyama vya upinzani kwamba wagombea wao pekee ndiyo waliowekewa pingamizi yana lengo la kuwahadaa watanzania.

Makalla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2024, ambapo alisisitiza CCM ipo tayari kushiriki uchaguzi huo na kitaibuka mshindi kwani kimejiandaa ipasavyo.
Fala sana sana
 
Back
Top Bottom