Makadirio ya tiles

Habari zenu! Kwa mafundi au mtu yeyote mwenye uzoefu, naomba kujua nyumba ya vyumba vinne inachukua tiles kiasi gani? Just makadirio.
Nyumba ina square meter ngapi? Na unataka utumie tiles za size gani (mfano 30cm×30cm,40cm×40cm n.k)...hivyo ndio vitu vya msingi kuvijua
 
Tafuta fundi aje akupimie akupe hesabu. Sio lazima ajenge yeye. Utapata uhalisisa zaidi.
 
Nyumba ina square meter ngapi? Na unataka utumie tiles za size gani (mfano 30cm×30cm,40cm×40cm n.k)...hivyo ndio vitu vya msingi kuvijua
angeweza kujua nyumba ina square meters ngapi angeweza kukadiria idadi ya tiles. labda aseme tu dimensions za hiyo nyumba tumsaidie.
 
Habari zenu! Kwa mafundi au mtu yeyote mwenye uzoefu, naomba kujua nyumba ya vyumba vinne inachukua tiles kiasi gani? Just makadirio.
Kila eneo nyumbani kwako litakuwa na tiles tofauti na eneo litakuw na ukubwa tofauti.
Mfano chooni,jikoni,sebuleni,vyumbani.
Box la tiles huwa linapimwa kwa sqm.
Mfano chumba chako ni 4m*4m maana yake ni 16sqm. Na unataka kutumia tiles za 40cm*40cm. Hizi box moja huwa ni 1.92sqm.
16/1.92=8.3 hapo utatumia box 8 na kipande,itakubidi ununue box 9.
Tumia kanuni hii nyumba nzima.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom