Majukumu muhimu ya Bunge ni kuandaa, kutunga (kupitia, kurekebisha na kufuta) sheria pamoja na kusimamia utendaji wa Serikali. Katika demokrasia, Wabunge hutekeleza majukumu hayo kama wawakilishi wa watu.
Ili kutekeleza majukumu yake muhimu, chombo cha kutunga sheria, lazima kiwe taasisi mathubuti yenye madaraka na uwezo wa kuzuia maamuzi ya Mamlaka ya utendaji (Serikali) na kuhakikisha kwamba Mtendaji (Serikali) anafanya hivyo kwa uwazi na uwajibikaji. Kwa kufanya hivyo Bunge utekeleza wajibu wake kwa "usawa na uwajibikaji".
Bunge huru na lenye meno, huhitaji nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi:
1) Rasilimali mali (majengo, miundo mbinu, mitandao, nk)
2) Rasilimali watu (wenye taaluma mbalimbali, ujuzi na uzoefu)
3) Asasi na utawala kusimamia na kuratibu shughuli za Bunge.
Je, bunge letu linajitosheleza kwa hayo, kiasi cha Wabunge na baadhi ya wananchi kutaka lioneshwe "live"!
Pia kuna masuala yafuatayo yanayowagusa wabunge moja kwa moja:
1) Uwakilishi bungeni uliotukuka.
2) Uwezo na kiwango cha Bunge kuisimamia Serikali.
3) Uwezo wa Bunge kutunga sheria.
4) Uwazi na upatikanaji wa taarifa za Bunge.
5) Uwajibikaji wa Bunge na Wabunge
6) Kiwango cha Bunge kujihusisha na Sera za Kimataifa.
Bunge letu linafikia kiwango gani katika hayo, ili suala la kuoneshwa "live" lipewe kipaumbele.