Maji ya kuchemsha na maji ya chupa yapi ni salama zaidi na yenye afya? Ni sawa kuchemsha maji ya kunywa kwenye birika ya umeme tofauti na sufuria?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,245
Habari yenu ndugu zangu,

Maji ya kuchemsha na maji ya chupa yapi ni salama zaidi na yenye afya?

Je, ni sawa kuchemsha maji ya kunywa kwenye birika ya umeme tofauti na kawaida tulivyozoea kuyachemsha kwenye sufuria kwa jiko la gesi au mkaa?
 
Hayo ya kuchemka yote yanafika 100 degrees kwahiyo ni sawa.

Ya chupa ni salama ila itategemea unayoyachemsha yametoka chanzo gani, yanaweza kua salama zaidi.
 
Kwangu mimi naona ya kuchemsha ikiwa yataandaliwa na kuhifadhiwa vizuri ni salama zaidi kuliko ya chupa ambayo purification ama tuseme treatment yake inahusisha mambo mengi kitu ambacho naona sio salama sana.

N.B mmewangu hata umdanganyeje ye anakunywa ya chupa tu
 
Me naona yakuchemsha, haya ya chupa ukinywa usiku halafu yabaki asbh ukiyanywa yanakuwa machungu hata sijui kwa nini.
Sasa umegusanisha na mdomo wako wenye mate bacteria wakatumbukia ndani ya maji chupani so vile vijidudu vinazaliana kuliko speed uijuayo na vingine vidadedi humo ndani ya maji so vinaozeana ndio harufu uikutayo na uchungu unaouona. Kkama wataka yawe poa maji ya chupa fungua kisha mimina kwenye chombo kingine unywe ile chupa iwe salama kutokana na bacteria wa kwenye mdomo wako.
 
Ni mwaka wa 13 sasa nachemsha maji,na ya dukani naona kama huwa hayanikati kiu
 
Maji yana mambo mengi sana na ukitaka kuyajua maji issues zake chukua vipimo. Maji ya Bomba yana almost kila takataka, kuna Mavi, Chumvi, udongo, kutu, chuma, sumu, mikojo, acid, backeria wazuri na wabaya ukitaka kuchunguza unaweza toka nduki. So kunywa yeyote tu sababu uwezo wetu ni mdogo muhimu ule vizuri uwe na afya kazi za figo, maini vifanye kazi vizuri kusafisha sumu na takataka mwilini.

Pia mwili pia unahitaji bacteria wazuri na wabaya ili kulindana kutokana na zamu za ulinzi wa mwili... ukinywa maji masafi sana nayo ni shida pia.

Maji ya chupa na dawasa mnayokunywa tizama picha down. baada ya kupimwa tena maji ya chupa ni hatari zaidi yana particals pia za plastic na unashauriwa usirudia kutumia chupa au chomba chepesi cha plastics sababu utakuwa unakunywa na kula chembe chembe plastic. Wale mnywao juice ziwekwazo kwenye chupa za maji be careful

1662406477495.png
 
Maji ya chupa kunywa mara moja moja hasa huku kwetu sehemu za joto. Yana kemikali nyingi na microplastics ambazo ndiyo kwanza wanasayansi wanajifunza madhara yake. Chuja na chemsha maji ya kunywa hasa haya ya kutoka visimani utakuwa unakunywa maji safi na salama sana!
Screenshot_20220905-152623_Chrome.jpg

Screenshot_20220905-152726_Chrome.jpg

Ya kuchemsha yana ukakasi mimi binafsi nikichukua lile chupa kubwa la Afya kwa jero najikuta mwamba.
Vipi kama ni kwenye familia ya watu say 6?? Mnanunua kila siku? Tatizo lililopo mfano maji ya bomba Morogoro kuna wakati ukifungua ni tope tupu so ni hatari sana kuyanywa bila kuchemsha. Miaka ya nyuma maji ya bomba yalikuwa well treated kiasi kwamba ulikuwa unaweza kukinga na kunywa moja kwa moja toka bombani..
 
Maji ya chupa kunywa mara moja moja hasa huku kwetu sehemu za joto. Yana kemikali nyingi na microplastics ambazo ndiyo kwanza wanasayansi wanajifunza madhara yake. Chuja na chemsha maji ya kunywa hasa haya ya kutoka visimani utakuwa unakunywa maji safi na salama sana!
View attachment 2346936
View attachment 2346937
Una undugu na Jesca Brown maana kiingereza kingi?
 
Maji yana mambo mengi sana na ukitaka kuyajua maji issues zake chukua vipimo. Maji ya Bomba yana almost kila takataka, kuna Mavi, Chumvi, udongo, kutu, chuma, sumu, mikojo, acid, backeria wazuri na wabaya ukitaka kuchunguza unaweza toka nduki. So kunywa yeyote tu sababu uwezo wetu ni mdogo muhimu ule vizuri uwe na afya kazi za figo, maini vifanye kazi vizuri kusafisha sumu na takataka mwilini.

Pia mwili pia unahitaji bacteria wazuri na wabaya ili kulindana kutokana na zamu za ulinzi wa mwili... ukinywa maji masafi sana nayo ni shida pia.

Maji ya chupa na dawasa mnayokunywa tizama picha down. baada ya kupimwa tena maji ya chupa ni hatari zaidi yana particals pia za plastic na unashauriwa usirudia kutumia chupa au chomba chepesi cha plastics sababu utakuwa unakunywa na kula chembe chembe plastic. Wale mnywao juice ziwekwazo kwenye chupa za maji be careful

View attachment 2346939

Kwaiyo chief wangu, chupa ya maji safi nayotumia kuwekea maji ya kuchemsha na kisha kuyanywa kutumia chupa hiyo ni kosa? Maana kila siku natumia chupa hiyo iyo.
 
Kwaiyo chief wangu, chupa ya maji safi nayotumia kuwekea maji ya kuchemsha na kisha kuyanywa kutumia chupa hiyo ni kosa? Maana kila siku natumia chupa hiyo iyo.
Mkuu chupa za plastic zina quality zake ila hizi zinazotumiwa na wauza maji ni for one time use only... maana baadae ni disaster tupu ikiwepo cancer na sumu tu mwilini kujipatia.
 
Back
Top Bottom