Majeneza ya kisiasa yasiyo na watu na hatma ya Taifa

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,766
12,689
Mwenyezi Mungu ametupa macho na ufahamu ili tusifanye makosa hayo tena. History inatuambia hakuna mahali popote mauwaji ya kisiasa yalileta amani au mataifa hayo kuwa nabutulivu.

Mauaji yakisiasa ni sawa na time boom 💥 ndio maana ma diktator wengi walikufa vifo vibaya au mataifa mengi yameanguka kwa sababu ya dam mara nyingi inasema na huwa inadai haki.

Kwa wale ni wasomi wa Bible mtakumbuka dam ya kaini ilivyo anza kumlilia Mungu mpaka Mungu akamwambia Habili dam ya ndugu yako yanililia.

Habili alipo muuwa ndugu yake hakujuwa kile kitatokea na huwo ndio ukawa mwanzo wa dam nyingi kumwagwa.
Dam ya watu wa Taifa yaweza kugeuka nakuwa chanzo cha mtikisiko wa taifa lolote duniani.

Sadam aliwauwa Kurdishi minority kama panya kwa kuwapylizia sumu nakufikiri angekuwa salama ila ile dam ya kurdishi haikumuacha salama hata baada ya miaka kadhaa na yeye alikuja kufa kifo cha aibu kutokana na mauwaji yale.

Sote tuna kumbuka Libya chini ya mkono wa chuma wa Ghadafi nchi ilisimama ila mauwaji ya wananchi wake na jinsi alianzisha mfumo wakupoteza watu taifa lilimlipukia na mwisho kuuwawa na watu wake na mpaka leo taifa halijapoa.

Mauwaji na dam ya Patrick Lumumba dam ilio mwagwa na wakongo wenyewe imebaki kuwa mwiba wa moto mpaka wa leo tangu kuuwawa kwake mpaka leo Kongo haija tulia.

Nini yatupasa kujifunza sisi watanzania na vyombo vya ulinzi na usalama nikuwa sio kila dam ni yakumwaga kuna dam mtamwaga na zitaliletea taifa shida na mateso huko tuendako.

Nikweli usio pingika uhaini ndani ya Taifa lako ni dhambi isiyo kuwa na msamaha. Niukweli usio pingika uhaini ndani ya Taifa lako adhabu nikifo na kifungo cha maisha. Lakini embu tutafakari inakuwaje siasa zetu za ndani zina leta machungu, visasi na hata mageneza yasio na watu yes majeneza yasio na watu ambayo watu wao wataomboleza mpaka Yesu arudi.

Je tulijiandaa na siasa za vyama vingi au vyama vingi vimekuwa trap kwa walio radical nakuwapoteza je tumewahi jiuliza gharama za hayo yote kwa mtu binafsi na Taifa?

Najuwa mkono wa serikali nimrefu na sisi sote nikondoo au kuku ktk banda ila ila tuingalie kesho maana ipo siku mageneza haya yataziba njia ipo siku mejeneza haya yataifunga kesho ya Taifa hili nakutuweka kwenye mkwamo na mbaya kuliko yote wakati huwo wengi wetu na walio tekeleza unyama huwo watakuwa wamesha lala.

Nilazima tuzuwie dam ya watanzania kumwagika pasipo sababu. Nilazima tuangalie aina ya dam inamwagwa yule mzee wa Tanga kweli sitaki kuamini walio muuwa wapo hai dam ya mzee kama yule kweli? Dam ya wazee kumwagwa ni laana kubwa sana well hatujuwi nini kilimkuta ila inatisha sana.
 
Mwanzilishi wa kuvuruga amani na utulivu wa nchi hi ni mzee wa chato kwakulinda chama chake na uongozi wake,leo yuko wapi?nashndwa kuamini kwnn haya yanaendelea? huyu wa sasa hajajifunza kwa mwenzake? damu ya watu ni laana.huwezi kulinda utawala wako kwa kumwaga damu za watu,lazima utaleta laana ndani ya nchi
 
Viongozi au tuseme watawala wetu jamani tafakarini kwa kina MAMBO yenye madhara haya ili MUNGU akupeni baraka .
 
Yule Marehemu kutoka Chato alaaniwe kama ilivyolaaniwa ARDHI ya sodoma na Gomora kwa ubaya aliouanzisha yeye na Genge lake kwa kuteka na kuua watu ila Adhabu yake alishailipia mapema Sasa imebaki kwa makombokombo aliyoyaacha yanayofanana na tabia zake
 
Nimesoma andiko lako lote neno kwa neno na mstari kwa mstari.lakini napingana na Baadhi ya maneno yako ambayo yanaharibu kabisa andiko lako zima.

Unaposema kuchagua na kuangalia aina ya Damu za kumwagwa unakuwa unamaanisha nini? Je Damu zipi zinatakiwa na kustahili kumwagwa na zipi hazistahili?

Nani anayepima ,kuthibitisha ,kuidhinisha na kutoa ruhusa ya kuwa Damu hii imwagwe na ya huyu isimwagwe au imwagwe kidogo?

Huyo mtu anatumia kigezo kipi kutoa idhinisho juu ya Damu ipi imwagwe na ipi isimwagwe? Huo mfumo wa kumwaga Damu za watu unasimamiwa na nani? Kwa sheria zipi? Kwa katiba ipi? Kwa mahakama ipi? Na kwa mamlaka ipi?

Kwanini kama mtu kafanya kosa asipelekwe tu mahakamani ili mahakama iamue? Kwanini Damu zingine zimwagwe kifichoni bila kufikishwa mahakamani na watu kusikiliza mwenendo mzima wa kesi na ushahidi wake?

Kwanini usingetoa ushauri wa kuwa hakuna anayestahili kumwaga Damu ya mtu yeyote yule wala kukatisha uhai wa yeyote yule na wala haitakiwi vitendo hivyo kufanyika hapa Nchini?

Kwanini unaziweka Damu za watanzania katika madaraja? Kwamba huyu Damu yake inastahili kumwagwa kutokana na makosa haya na huyu haitakiwi kumwagwa? Vipi kama mtoa idhini,ruhusa na mamlaka akatoa na kuruhusu kumwagwa kwa Damu ya mtu fulani kwa chuki zake tu binafsi au kwa kulinda cheo chake? Nani atarudisha uhai wa huyu aliyeonewa? Maana kama ni mahakamani kuna kukata rufaa na hatimaye mtu kupata haki yake.

Ningependa kukwambia na kukushauri kuwa usiweke Damu za watanzania katika madaraja wala usiwe mtoa hukumu ya kuwa huyu anatakiwa kuuwawa na huyu hastahili. Ni lazima tuseme kuwa hakuna mwenye haki ya kutoa wala kukatisha uhai wa mtanzania yeyote yule bila kujali itikadi za kisiasa au sababu ya aina yoyote ile. Ni lazima utawala wa sheria uzingatiwe na siyo watu kujichukulia sheria mkononi.

Kama mtu ana kosa la aina yoyote ile basi afikishwe mahakamani na ushahidi utolewe juu ya makosa ya mhusika na uamuzi ufanyike.haki itendeke na ionekane imetendeka.

Ni lazma tukatae Damu ya mtu yeyote yule kumwagwa.iwe ni ya kijana au mzee au mwanamke au mwanaume au Raia wa kawaida au Albino au vyovyote vile ni lazima tusema HAPANA kumwaga Damu katika ardhi yetu. Tusipande laana katika ardhi yetu na kuleta mikosi na nukusi hapa Nchini.

Mwisho naomba upitie maandiko yako yote ya siku za nyuma uone ulichokuwa ukiandika siku za nyuma na uone kama ulikuwa sahihi na vipi watu wanakuchukuliaje kwa sasa hasa unapotoa andiko kama hili.

Naweka kalamu yangu chini .nitakuja kushusha hoja zingine hapa .ngoja kidogo.
 


Umeandika vizuri Sana Leo
 

Kwakuwa nchi yetu inaendeshwa Kwa sheria tunabidi kuheshimu damu ya kila Mtanzania .
 
Kauli za kisiasa na uhaini vina mahusiano Gani?
 
Naona kama huu ni unafiki mkubwa sana vile, huko uliko kwenye chama chako cha siasa wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo Mambo haya yote ambayo umeeleza kwa kuyapinga hapa.
 
Habili alipo muuwa ndugu yake hakujuwa kile kitatokea na huwo ndio ukawa mwanzo wa dam nyingi kumwagwa.
Dam ya watu wa Taifa yaweza kugeuka nakuwa chanzo cha mtikisiko wa taifa lolote duniani.
Waleze ndugu zako Choicevariable, chiembe, Tlaatlaa, kipara kipya na Faizafox sisi tunayajua.
 
Bora mmekutana wenyewe kwa wenyewe ngoja tuone itaishia wapi
 
Mkuu TumainiEl Ahsante sana kwa andiko hili makini. Lakini naomba hapo kwenye mfano wa Habili kumuua Kaini ubadilishe, iwe Kaini kumuua Habili.
Vinginevyo, ahsante sana kwa kuwatahadharisha viongozi wetu ili watumie nafasi zao vizuri..
Kwamba maneno matupu kama haya yanawatisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…