Jana nilipanga leo nianzishe thread ya kushauri mradi wa DART. Bahati mbaya ama nzuri nikiwa nasikiliza magazeti asubuhi nikasikia kuhusu kuanza kwake.
Nilitaka kushauri kwamba tukiwa tunasubiria majadiliano ya nauli na mwekezaji, na kwa kuwa barabara ni yetu na sio ya mwekezaji, na kwa kuwa hatujui majadiliano yatachukua muda gani, nilitaka kushauri kwamba daladala za kawaida ziruhusiwe kutumia barabara hizo kwa kipindi cha mpito. Watu wanachulewa maofisini kwa ajili ya foleni wakati wangeweza kuwahi ikiwa daladala zingeruhusiwa kutumia miundombinu hiyo. Aidha, ingepunguza foleni hata kwa private cars kwny barabara za kawaida. Barabara ya DART ni yetu, sio ya mwekezaji. Sioni mantiki ya kumsubiri mwekezaji na bei zake za kibepari. Tungeanza na mabasi yetu ya kaida kwa kuyasimamia vizuri yatumie barabara za mradi.
Yalikuwa mawazo yangu lakini nadhani yamechelewa ikiwa kweli mabasi ya mradi yataanza next week.