Tupo na jamaa zangu kijiweni, tukifanya mazungumzo kuhusu soka. Ghafla mmoja wetu akatokea na kusema, "Unajua, mama anaupiga mwingi sana, hasa kwenye suala la kununua goli moja kwa milioni tano!"
Mwingine alihitaji ufafanuzi, akahoji, "Anaweza kununua magoli kisha anayauzia wapi?" Kabla ya kupata majibu, mwingine akajibu, "Labda anaweka kwenye maktaba ya Ikulu kama kumbukumbu!"
Mwanzisha mada alijitokeza na kusema, "Si hivyo ndugu zangu. Mama anafanya hivyo ili timu zetu ziwe na nguvu za kufanya vizuri kimataifa."
Mtu mwingine akainuka na mtazamo wake, akasema, "Vipi kuna ulazima wa kununua hayo magoli bora? Ingekuwa bora angeendelea kutukopesha vijana kwa masharti nafuu, kisha tunazirudisha serikalini fedha hizo. Hali hii inatufanya tushindwe kuelewa faida ya matumizi haya ya fedha za magoli."
Soma Pia: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF
Nilijikuta nikiondoka baada ya kuona mjadala umekuwa mzito, ghafla nikasikia mtu ananiita, "Bwana Kaduga, mbona unaondoka bila kusema chochote?" Nilipogeuka niseme neno lolote, niligundua kuwa nilikuwa nikistuka kutoka usingizini.