Majadiliano ya kijamii kuhusu ununuzi wa magoli na athari zake katika soka tanzania

Bwana kaduga

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
863
1,811
Tupo na jamaa zangu kijiweni, tukifanya mazungumzo kuhusu soka. Ghafla mmoja wetu akatokea na kusema, "Unajua, mama anaupiga mwingi sana, hasa kwenye suala la kununua goli moja kwa milioni tano!"

Mwingine alihitaji ufafanuzi, akahoji, "Anaweza kununua magoli kisha anayauzia wapi?" Kabla ya kupata majibu, mwingine akajibu, "Labda anaweka kwenye maktaba ya Ikulu kama kumbukumbu!"

Mwanzisha mada alijitokeza na kusema, "Si hivyo ndugu zangu. Mama anafanya hivyo ili timu zetu ziwe na nguvu za kufanya vizuri kimataifa."

Mtu mwingine akainuka na mtazamo wake, akasema, "Vipi kuna ulazima wa kununua hayo magoli bora? Ingekuwa bora angeendelea kutukopesha vijana kwa masharti nafuu, kisha tunazirudisha serikalini fedha hizo. Hali hii inatufanya tushindwe kuelewa faida ya matumizi haya ya fedha za magoli."

Soma Pia: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Nilijikuta nikiondoka baada ya kuona mjadala umekuwa mzito, ghafla nikasikia mtu ananiita, "Bwana Kaduga, mbona unaondoka bila kusema chochote?" Nilipogeuka niseme neno lolote, niligundua kuwa nilikuwa nikistuka kutoka usingizini.
 
Hili jambo limekaa kisiasa zaidi.

Anyways, Jukwaa la Simba na Yanga ni sehemu yenye nguvu zaidi kwa watanzania, baada ya nyumba za ibada.
 
Yuko kuhamasisha utalii wa michezo hizi team zinapofanya vizuri utalii kupitia michezo unaongezeka na pato la taifa na mtu mmoja mmoja kuongezeka
Waarabu wamechelewa kujua hili Sasa wanapambana ila Uingereza soka ni bidhaa inayowaingizia pato kubwa na kuajiri watu wengi
 
Tupo na jamaa zangu kijiweni, tukifanya mazungumzo kuhusu soka. Ghafla mmoja wetu akatokea na kusema, "Unajua, mama anaupiga mwingi sana, hasa kwenye suala la kununua goli moja kwa milioni tano!"

Mwingine alihitaji ufafanuzi, akahoji, "Anaweza kununua magoli kisha anayauzia wapi?" Kabla ya kupata majibu, mwingine akajibu, "Labda anaweka kwenye maktaba ya Ikulu kama kumbukumbu!"

Mwanzisha mada alijitokeza na kusema, "Si hivyo ndugu zangu. Mama anafanya hivyo ili timu zetu ziwe na nguvu za kufanya vizuri kimataifa."

Mtu mwingine akainuka na mtazamo wake, akasema, "Vipi kuna ulazima wa kununua hayo magoli bora? Ingekuwa bora angeendelea kutukopesha vijana kwa masharti nafuu, kisha tunazirudisha serikalini fedha hizo. Hali hii inatufanya tushindwe kuelewa faida ya matumizi haya ya fedha za magoli."

Soma Pia: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Nilijikuta nikiondoka baada ya kuona mjadala umekuwa mzito, ghafla nikasikia mtu ananiita, "Bwana Kaduga, mbona unaondoka bila kusema chochote?" Nilipogeuka niseme neno lolote, niligundua kuwa nilikuwa nikistuka kutoka usingizini.
Hadithi, (story), za vijiweni huishia vijiweni, kwa ulivyo andika inatafsiri aina ya watu, (caliber), mlioko kwenye kijiwe chenu,

Life learning skills is very important for an individual, to help interpret what is going around in society
 
Yuko kuhamasisha utalii wa michezo hizi team zinapofanya vizuri utalii kupitia michezo unaongezeka na pato la taifa na mtu mmoja mmoja kuongezeka
Waarabu wamechelewa kujua hili Sasa wanapambana ila Uingereza soka ni bidhaa inayowaingizia pato kubwa na kuajiri watu wengi
Mahesabu rahis,i uwanja wa mkapa unachukua watu 60,000 fanya kima cha chini cha kiingilio uwanjani kiwe elfu 3 inamaanisha ukijazwa zitapatikana milioni 180. Je ni ving"amuzi vingapi vya Azam tanzania nzima vinavyo oneshesha mpira piga kwa mwezi wanalipia 28,000 serikali inapata kiasi gani? Kwa mwezi na kwa siku?

Kwa maneno mengine hizi hela zinarudi kilaini sana, ninamna nzuri ya kurudisha fedha kwa wale waliosababisha ziingie
 
Umefafanua ki uchumi zaidi binafsi nilibaini sports tourism inalipa sana ndio maana mataifa makubwa yanawekeza huko na kwenye kumbi kubwa za makongamano e.g Kigali convention center
 
Shida ya watanzania ni ujuaji na wanaleta ujuaji ata ktk mambo wasoyajua
Ntakupa mfano kila mtu asokua kwenye sekta ya utalii aliponda sinema ya mama ila tulioko kwenye sekta ya utalii kwa sasa tunaona na kuonja mafanikio ya ile sinema yake

Tangu mwez wa nne mwaka huu ktk ofs zetu wazungu ni weng saiv tunashika dola tu japo sio nying sana ila saiv dola tunazishika sana miaka ya nyuma season huwa inaanza mwez wa5 ad kufka wa 9 inaanza pungua ila saiv wazungu ni weng sana

Sometimes vijana wa kitanzania ni wajuaji na waongeaji sana kwa ufupi ni watu wa lawama lawama tu saiv serikal inatoa pesa nying sana za vikundi vya vijana tena ad million20+ kwa kikundi mbona hawajaenda wakajiunga vikundi wakapewa izo pesa kwaiyo pesa wanazokopesha na izo pesa za gori la mama utofauti nn

Tuache lawama na majungu vijana wa kitanzania na ndo maana tunaendelea kutawaliwa na CCM kwasababu ya ujinga na chuki binafsi zilizotujaa
 
Back
Top Bottom