Maiti kugoma kuzikwa mpaka mahari itolewe

Selemani Sele

JF-Expert Member
Feb 25, 2023
314
693
Kama mtembezi wa mtaani nimeshuhudia jambo ambalo limenishangaza na kunistaajabisha kwa wakati mmoja na hii ni mara ya mbili kuliona hapa vingunguti je ni jambo gani? Kaa chonjo.

Ni hivi ndugu wa mke au mume kuforce kufunga ndoa na maiti

Ilikuwa juzi wakati nahangaika na shughuli zangu za kujenga taifa nikaona ndugu wamemshikia panga mwanaume kwenye msiba wa mke wake ambaye walifanikiwa kupata watoto wanne ila walikuwa hawajaoana sasa ndugu wakasema hawaziki mpaka atoe mahari na amuoe yule marehemu bwana akafikiri utani ila alikaliwa kooni mpaka ndugu wakajichanga na kutoa mahari ndo maiti ikaruhusiwa kuzikwa.

Nyingine nilipata taarifa au uitwavyo umbea kutoka kwa jirani yangu kwamba ndugu walikuwa kanisani wanasubiri maiti iingie isaliwe kwa ajili ya mazishi ambapo ndugu wa mke walitinga na vurugu kwamba ndugu yao hazikwi mpaka mahari itolewe yaani ilikuwa vurumai vurugu tupu mpaka aibu aseee, ndugu wa mme aliyefiwa walichanga milioni 2 na vitu vingine alitakiwa awasilishe, baada ya hapo ndo marehemu walienda kuzikwa.

Je ushawahi kushuhudia kama mimi utupe story yako.Tushee idea mbali mbali

Wako selemani sele.

Jamii forums news update nimepata link inayoshabiana na hii ishu.

Aibu ya mwaka: Kumbe mahari ina umuhimu sana
 
Sasa wewe kwanini usifuate utamaduni wa sehemu husika (when in Rome do as Romans) wazee hao kwa tamaduni zao lazima utoe mahari sio kwamba ni masikini bali ni utaratibu kwahio ukikiuka yatakukuta ya kukuta kuna wazee wakorofi wanaweza wakakurudisha na maiti yako (kwao ni kama vile uliiba mtoto wao)
 
Sasa wewe kwanini usifuate utamaduni wa sehemu husika (when in Rome do as Romans) wazee hao kwa tamaduni zao lazima utoe mahari sio kwamba ni masikini bali ni utaratibu kwahio ukikiuka yatakukuta ya kukuta kuna wazee wakorofi wanaweza wakakurudisha na maiti yako (kwao ni kama vile uliiba mtoto wao)
Kwenye msiba kweli kwann wasisubir
 
KAMA MTEMBEZI WA MTAANI NIMESHUHUDIA JAMBO AMBALO LIMENISHANGAZA NA KUNISTAAJABISHA KWA WAKATI MMOJA NA HII NI MARA YA MBILI KULIONA HAPA VINGUNGUTI JE NI JAMBO GANI? KAA CHONJO.

NI HIVI NDUGU WA MKE AU MUME KUFORCE KUFUNGA NDOA NA MAITI
ILIKUWA JUZI WAKATI NAHANGAIKA NA SHUGHULI ZANGU ZA KUJENGA TAIFA NIKAONA NDUGU WAMEMSHIKIA PANGA MWANAUME KWENYE MSIBA WA MKE WAKE AMBAYE WALIFANIKIWA KUPATA WATOTO WANNE ILA WALIKUWA HAWAJAOANA SASA NDUGU WAKASEMA HAWAZIKI MPAKA ATOE MAHARI NA AMUOE YULE MAREHEMU BWANA AKAFIKIRI UTANI ILA ALIKALIWA KOONI MPAKA NDUGU WAKAJICHANGA NA KUTOA MAHARI NDO MAITI IKARUHUSIWA KUZIKWA.

NYINGINE NILIPATA TAARIFA AU UITWAVYO UMBEA KUTOKA KWA JIRANI YANGU KWAMBA NDUGU WALIKUWA KANISANI WANASUBIRI MAITI IINGIE ISALIWE KWA AJILI YA MAZISHI AMBAPO NDUGU WA MKE WALITINGA NA VURUGU KWAMBA NDUGU YAO HAZIKWI MPAKA MAHARI ITOLEWE YAANI ILIKUWA VURUMAI VURUGU TUPU MPAKA AIBU ASEEE, NDUGU WA MME ALIYEFIWA WALICHANGA MILIONI 2 NA VITU VINGINE ALITAKIWA AWASILISHE, BAADA YA HAPO NDO MAREHEMU WALIENDA KUZIKWA.

JE USHAWAHI KUSHUHUDIA KAMA MIMI UTUPE STORY YAKO.TUSHEE IDEA MBALI MBALI
WAKO SELEMANI SELE.
JAMII FORUMS NEWS
Tamaduni za Wazungu zimekuja kufanya Tamaduni za kiafrica zionekane ni ujinga....ila sivyo
 
Hiyo ndio habari ya mjini, wewe ishi na mtoto wa mtu haujamalizana na upande wa kwao, siku akikufa utalipa labda uombe utangulie wewe
 
Back
Top Bottom