Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Watanzania tunapenda sana kutengeneza habari za uongo. Ni kipaji fulani kisichofaa kuwa sifa ya mtu lakini ndio ukweli kwamba tunacho na tunapenda kukiendeleza.
Uvumi unaweza kusambaa haraka sana mpaka mhusika anapokuja kukanusha tayari habari zinakuwa zimeshambaa kila kona na uongo wa kutungwa unakuwa ndio ukweli. Labda ni ukosefu wa kazi unaotusumbua siku zote!.
Labda ni ukosefu wa elimu unaotunyima fursa ya kutafakari jambo kwa kina na kuona kama kinachosemwa ni cha kweli au ni cha uzushi, au labda ni robo mbaya tu inayochanganyika na wivu inayotusumbua.
Hapa Mbezi Beach yapo majengo mawili yenye kufanana, moja limeshamalizika na linatumiwa kama ukumbi wa shughuli za harusi linaitwa SEA BREEZE HILL na lingine bado linajengwa halijamaliziwa. Ukiwa unatoka mjini kuelekea daraja la apson utayaona yapo kushoto kwako na kulia utaona maghorofa ya BOT. Kwa muda mrefu tu inavumishwa kwamba ni mali ya Ridhiwani Kikwete wakati ukweli ni tofauti kabisa na huo uvumi.
Yanamilikiwa na Mzee fulani mwenye hoteli yake mitaa ya Kariakoo karibu na kituo cha mabasi ya mwendo kasi, lakini uvumi uliovumishwa na watu wengi wakidhania ni ukweli ni kuwa yale maghorofa ni mali ya Ridhiwani mtoto wa JK, Hivyo wanaojenga hoja kuwa familia ya JK ina mali nyingi wanakuwa wamehesabu pia na hayo maghorofa!!.
Ni kama ambavyo zile maiti zilizokuwa zikiokotwa pale Coco Beach zilivyohusishwa na awamu ya JPM, watu wengi maskini ya Mungu wakajua ni hivyo!, kwamba JPM anawashughulikia wote wanaokwenda kinyume na matakwa yake.
Lakini awamu ya sita ikiwa inafikia nusu ya safari bado kuna miili ya watu inaokotwa ndani ya viroba sehemu mbalimbali za Tanzania, je hizi ni maiti zenye uhusiano na awamu ya tano?.
Unyama ni sifa ya binadamu, tuna roho mbaya sana siku zote. Hatufahami juu ya unyama wetu kwani vyombo vya habari havifiki kila sehemu na kuripoti matukio. Lakini kila siku kuna watu wanachinjwa, wanadhalilishwa na kuwekwa ndani ya viroba ni sifa mbaya ya binadamu.
Tulitenda dhambi ya kumsingizia JPM kuwa ni mtu mwenye kuondoa uhai wa watu, lakini mpaka kesho bado matukio yale yale ya awamu yake yanaendelea kutokea hapa nchini. Tuitubu hii dhambi vinginevyo itatuumiza sana huko tuendako.