mHAMAS-shaji
Member
- May 31, 2024
- 13
- 8
SEASON-1
EPISODE 01
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mmoja wetu kwa kufika hatua hiyo ya kumaliza elimu ya upili baada ya kumaliza mitihani ya kidato cha sita.
Kilichobaki kwa wakati huo ilikuwa ni kuagana👋 kwa kila mmoja wetu kwani tulijua ya kuwa hakuna kitu kingine cha kutukutanisha kwa namba kubwa kama ile tena, ilikuwa ni huzuni😥 miongoni mwetu kwani ule undugu tuliokuwa nao ndani ya miaka miwili ndiyo ulikuwa unakoma wakati huo.
Kwa kulitambua hilo lilitolewa wazo la kukutana pamoja katika shule hiyo wakati wa kufuata vyeti vya kidato cha sita pale vitakapotolewa na wazo hilo liliungwa mkono na kila mmoja wetu.
Kipindi zikiendelea ratiba za kuagana kwa kupeana namba za simu na namna nyingine nilitizama saa🕖 na kugundua kuwa nina wastani wa masaa mawili na dakika zipatazo tano kabla tiketi iliyopo mikononi mwangu haijaisha muda wake.
Nilishugulisha kichwa changu kwa dakika moja nikagundua kuwa nikilaza damu hela💰 yangu nitakuwa nimemchangia mwarabu kijinga hivyo nikaona mambo yasiwe mengi mana kwetu ni pazuri na nilikwishapakumbuka.
Niliwatizama wahitimu wenzangu nikawaona bado wanaagana huku wengi wao wakiwa hawana tiketi kama mimi kwani mabasi ya kwenda kwao hayakuwepo mchana huo kutokana na umbali wa route yao uliokuwa ukiwahitaji masaa zaidi ya kumi hadi kufika makwao tofauti na kwetu ambako yalinitosha masaa sita pekee.
Kitu ambacho nilikuwa nikikisikia kwao walikuwa wakipanga kwenda kituo cha mabasi majira ya jioni kwa ajili ya kukata tiketi kwani hakukuwa na utaratibu wa shule kuandaa usafiri wa pamoja kwa wahitimu maana kulikuwa na mchanganyiko michepuo ya sayansi, sanaa na uchumi hali iliyopelekea kutomaliza kwa wakati sawa tofauti na wakati wa likizo za mihula ambapo wanafunzi wote humaliza mitihani kwa pamoja siku ya Ijumaa na kusafiri pamoja alfajiri ya Jumamosi.
Nikagundua hapo sina wa kuondoka naye hivyo niliiba muda wangu kidogo kwakuchukua namba za simu kama tatu ikiwemo ya dada mmoja mwenye urembo wake aliyefahamika kwa jina la Zainabu Khamis binafsi nilikuwa nikimwita Zaimisi.
Kulikuwepo na utaratibu wa kuchafuliana shati za shule kwa kuwa zilikwishakumaliza muda wa matumizi hivyo kila aliyeona shati la mwenzake likiwa safi ama likiwa na sehemu ya kuandika pasi nakuombwa alimsogelea na kuchukua kalamu ya kawaida ama makapeni🖍 na kuchora alichojisikia.
Lengo kubwa la kufanya hivyo ilikuwa ni kupeana namba za simu📱 kwani hakukuwa na mwenye simu ya kuhifadhi namba maana hatukuruhusiwa kuzimiliki kipindi cha masomo,📚📖 lakini mbali na hapo tulifanya hivyo kama sehemu ya kutunza kumbukumbu kwa wanadarasa kwani tuliandika namba za simu na majina yetu pamoja na kuweka saini zetu.
Kwa upande wangu sikuona umuhimu wa kuchafua shati la yeyote kwani sikuwa nikimiliki simu wala namba yake lakini pia muda ulikuwa ukiniendea matiti, hivyo basi pasi na kuaga mdogomdogo nilianza kujongea kuelekea lilipo bweni lililofahamika kwa jina la Mikumi.
Nikiwa nimepiga hatua kadhaa nilisikia sauti nyororo ikitamka “Hallow K baby”.
Waooh alikuwa ni mwanangu wa nguvu mwanadada Linda, msichana mwenye PCM yake ingawaje michepuo yetu ilikuwa ni kulia na kushoto lakini mara nyingi tulikuwa tukijisomea pamoja.
“Nambie mamdogo”,
nilimjibu huku nikimsubiri kwwani tayari alikuwa akipiga hatua kuupunguza umbali uliopo baina yetu.
“Mbona kama unajitenga mwanangu wapi unaelekea”,
aliendelea kuniuliza nami nikamjibu
“Oooh mummy so sorry, I do have a ticket to home on my hand and it is going to expire soon so nawahi kujiandaa mana I think kuna lisaa limoja na dakika chache kabla bus halijang’oa nanga”.
Maneno yale yalionekana kumhuzunisha Linda niligundua hilo kupitia uso wake naye akasema
“Mkaka una roho mbaya wewe yaani umekata tiketi hujaniambia haitoshi unaamua kuondoka kimyakimya bila kunijuza”.
Linda alinitupia shutuma hizo ambazo zilinifanya nijione mkatili mbele yake japo sikutaka kuonesha unyonge nikajitetea kwa kusema
“Jamani Linda ndo unapoteza kumbukumbu hivyo mbona nilikwambia tangu juzi kuwa nikimaliza mtihani wa mwisho sitoweza kulaza mbavu zangu hapa nikawanufaisha kunguni”.
Aliendelea kuniambia “Sawa ulisema na hiyo tiketi ulikata saa ngapi nisijue?”
Nikamjibu “Ni kweli sikukwambia ila tiketi yenyewe nimeipata leo asubuhi nilimuagiza jana jamaa wa dukani alipokwenda mjini kufungasha ndo leo kabla sijaingia kwenye mtihani nikaipitia kwahiyo jana ilikuwa vigumu kukwambia maana bado sikuwa na uhakika kama amepata au vinginevyo, samahani lakini mhandisi mama yangu mdogo kama nimekukwaza”.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Itaendelea...........................