Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,206
- 1,465
GT habari za asubuhi.
Kampeni za mwaka huu viongozi wa dini ya KIKRISTO wameongoza kuvunja sheria na taratibu za uchaguzi kwa kuonesha bayana yule wamtakaye.
Hili linanikumbusha habari ya kuchaguliwa kwa mfalme Daudi kuwa mfalme wa Israel. Mambo yafuatayo yalijitokeza:-
1. Mungu alimtuma Nabii Samwel akampake mafuta mfalme wa Israel
2. Mungu alimtuma Nabii Samwel aende katika nyumba ya Yesse na kati ya vijana wake Mungu amemchagua mmoja kuwa mfalme.
3. Nabii Samwel alipowaendea wazee wa Bethlehem walistuka hata kumuliza Je kuna amani??? Na ndipo alipowaambia na tutoe dhabihu.
4. Wakati IBADA ilipoanza ndipo Nabii Samwel alipoanza kuchagua mfalme mpya kwa kufuata matamanio ya moyo wake na sivyo Mungu alivyotaka.
5. Mungu alimuonya Nabii Samwel asiangalie mwonekano mzuri, urefu wa mtu,nk kwani Mungu haangalii hayo.
Mungu haangalii kama mwanadamu anavyoangalia, haijalishi ni Nabii, Mtume, Mwalimu au Askofu.
6. Tabia ya Mungu ni kuangalia NIA YA NDANI (For The Lord does not see as man sees; for man looks at the outward appearance, but The Lord looks at the HEART) statement of fact.
Tafsiri - Mungu haangalii vile mwanadamu anavyoangalia, kwani mwanadamu anaangalia mwonekano wa nje lakini Mungu anaangalia MOYO).
7. Hivyo basi haijalishi nani katabiri nini, nani kahubiri nini? nani kasema nini. Bado mpango wa Mungu na kusudi la Mungu kwa Tanzania litasimama.
8. BWANA HUYABATILISHA MASHAURI YA MATAIFA, HUYATANGUA MAKUSUDI YA WATU, SHAURI LA BWANA LASIMAMA MILELE, MAKUSUDI YA MOYO WAKE VIZAZI NA HATA VIZAZI.
9. Mwisho tunaona Nabii Samwel akiulizia iwapo kuna kijana mwingine wa Mzee Jesse, na ndipo Daudi akachaguliwa kuwa mfalme.
10. Daudi hakuwa amejiandaa hata kidogo kuwa mfalme, bali ulikuwa ni mpango wa Mungu mwenyewe.
HITIMISHO
Viongozi wa dini wameamua waziwazi kutuhamasisha tumchague mtu fulani kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi hawa wamesahau wajibu wao kutuongoza kuomba ili Mungu amchague yule aliyeupendeza moyo wake.
Kuna viongozi waliolifanya hili wazi na wengine wametumia akili ila unaelewa moyo unakoelekezwa. Haya nimeyaona katika mahubiri ya safari hii ya Mwl MWAKASEGE.
Jambo hili sio geni hata Nabii Samwel alifanya haya haya na mwisho wa siku Mungu aliyakataa mapendekezo ya Nabii Samwel na ndipo Daudi akawa mfalme wa Israel. TENA AKAWA THE BEST LEADER BAADA YA WOTE WALIOMTANGULIA KUBORONGA.
KWA MAANA HIYO BASI, WATU WOTE TUINGIE KWENYE MAOMBI YA TOBA NA TUMUOMBE MUNGU ATUPE RAIS ALIYEUPENDEZA MOYO WAKE. USISAHAU KUSINDIKIZA MAOMBI YAKO NA SADAKA. Viongozi wa dini tuelekezeni kwenye maombi na sio kwenye majina ya watu. Let the will of God prevail.
EE MUNGU TUSAIDIE. EE MUNGU IBARIKI TANZANIA. EE MUNGU TUPE DAUDI.
QUEEN ESTHER
-------------------------------------------------------------------------
Ukisoma andiko langu vizuri UTAELEWA. Sina sababu ya kumchafua mtumishi wa Mungu Mwl. MWAKASEGE. In fact yeye ndie aliniombea ujazo wa Roho Mtakatifu.
Fanya utafiti wako utagundua majority ya wanaohudhuria mkutano wake tangu mwanzo wanatoka na majumuisho kuwa Mwl. anaonesha bayana kwamba chaguo ni Mhe. Lowasa. Jitahidi kufanya ka research kadogo utanielewa.
Inawezekana kuna haya yafuatayo:-
1. Mwalimu anatumia lugha ngumu watu hawamuelewi.
2. Inawezekana ana kundi la wasikilizaji wanywa maziwa na yeye anawapa MIFUPA.
3. Ni vizuri akatumia lugha nyepesi kwa audience aliyo nayo, naamini Roho Mtakatifu atamsaidia.
4. Mimi ni mmoja wa wanaomuombea ktk mahubiri yake. We pray for the guidance of the Holy Spirit and eloquent speech.
Mwisho ni vizuri kuliweka hili wazi ili ijulikane bayana kuwa MWL MWAKASEGE HANA JINA LA MGOMBEA.
Wote wanaopotosha hili kupitia mitandao ya kijamii na maofisini waache mara moja. Sisi yetu ni maombi Tanzania impate Daudi.
Asante kwa ushauri.