ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,891
- 69,610
My Take
Wachungaji wa Makanisa ya Voda fasta tafuteni kazi za kufanya badala ya kutapeli Waumini Kwa visingizio vya Zaka za bwana.
====
Mgogoro wa ama ni mkopo au sadaka ya fungu la kumi (zaka) baina ya Mchungaji John Mtuka wa Kimara na muumini wake, Neema Wawa umehitimishwa na Mahakama Kuu ikibainisha ni mkopo unaostahili kurejeshwa.
Muumini huyo alimfikisha mahakamani mchungaji huyo akimdai Sh15 milioni alizomkopesha, huku mchungaji huyo akidai fedha hizo hazikuwa mkopo, bali zilitolewa kama sadaka ya fungu la kumi kwenye kanisa wanaloabudu (halikutajwa), shauri ambalo limefika hadi mahakama kuu.
Hata hivyo, katika hukumu yake, Jaji John Nkwabi wa Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam, alisema fedha hizo, hazikuwa fungu la kumi wala sadaka ya ujenzi kama mchungaji alivyokuwa anaeleza, bali ulikuwa ni mkopo.
Hayo yamo katika hukumu ya Jaji Nkwabi iliyotolewa juzi kuhusu rufaa ya kesi iliyokuwa imekatwa na Mchungaji Mtuka, akipinga hukumu ya mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ya Agosti 2, 2022 iliyompa ushindi Neema Wawa.
Katika hukumu hiyo, Jaji Nkwabi alianza kwa kusema rufaa hiyo inashangaza kwa sababu wadaawa walikuwa na mahusiano ya mchungaji na muumini na muumini alikuwa akihudhuria kanisani ambako mchungaji aliweza hadi kufahamu ukwasi wake.
“Ilitokea pale uwezo wa kifedha wa mjibu rufaa (Neema) ulipokaa sawa, mrufani (mchungaji) alifahamu kupitia fungu la kumi alilokuwa akilitoa, suala ambalo kiukweli ndiyo mahitaji ya mafundisho ya dini,” alieleza Jaji.
“Wakati mchungaji anadai muumini wake alilipa Sh5 milioni kama fungu la kumi, muumini wake anasema alilipa tu Sh1 milioni kama fungu la 10. Kwa maoni yangu utata wa hii kesi ulianzia hapa, ukichanganya na madai ya michango ya ujenzi,” alisema.
Mwananchi