Mahakama yakubali kuutumia mkojo wa Masogange, yasema fomu za mkemia zilifata sheria

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,662
8,787
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea taarifa ya mkemia wa serikali iliyoonesha kwamba sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald "Masogange" una chembechembe za dawa za kulevya.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema leo kwamba pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali na mahakama imepokea taarifa hiyo ambayo itatumika kama ushahidi.

Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani. Pia amesema Polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo. *Kesi itaendelea kwa ushahidi baadae

CHANZO: Habari Leo

=====

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Back
Top Bottom